OPERESHENI ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Joseph Magufuli kuhakikisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inakusanya kodi ipasavyo imeiweka soka ya nchi hii katika msukosuko kidogo.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limelazimika kusitisha ziara ya timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15 (U-15) nchi za Afrika Mashariki, kutokana na kutikiswa na TRA baada ya akjaunti zake kufungwa kwa sababu ya kodi.
Wiki iliyopita U-15 iliagwa kwa ziara za Burundi kupitia Kigoma, Rwanda, Kampala, Uganda na Kenya, lakini sasa watageuzia Mwanza baada ya mtikisiko huo, kufuatia TRA ya Ilala kuzuia fedha kwenye akaunti zote za TFF kwa madai ya kulipwa kiasi cha Shilingi 1,637,334,000 (bilioni 1.6 tshs) ikiwa ni kodi kwa kipindi cha 2010 – 2013 sehemu kubwa ikiwa ni makato kwenye mishahara (PAYE) ya walimu wa kigeni, Jan Poulsen, Kim Poulsen na Jacob Michelsen na vilevile kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye mchezo wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) dhidi ya Brazili uliofanyika mwaka 2010.
Walimu wa Timu za Taifa wamekuwa wakilipiwa mishahara na Serikali na hivyo TFF haikuwajibika kuwakata kodi. Aidha, mchezo kati ya Tanzania na Brazil ulisimamiwa na kamati maalum ya Serikali na fedha zake hazikuingizwa katika akaunti za TFF.
Kutokana na hatua hii ya TRA shughuli nyingine za mpira zitakazohathirika nazo ni:
1. Kulipia madeni ya usafiri, chakula na posho za Timu za Taifa zilizoshiriki mtoano wa kombe la Dunia na mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (Challenge Cup)
2. Program za mpira wa Wanawake na vijana zitalazimika kusimama.
3. Mashindano ya kombe la Shirikisho raundi ya pili iko kwenye hatihati kwani hakuna fedha za kugharimia michezo hiyo.
4. Mashindano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) inayoendelea yatalazimika kusimama vilevile. Mashindano haya TFF imekuwa ikiyaendesha bila mdhamini.
5. Vifaa vya michezo (Mipira) kwa ajili ya shule za msingi na vituo vya maendeleo (Regional Football Development Centres) vinatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote na TFF haitakuwa na uwezo wa kulipia usafirishaji na ushuru wake.
6. Malipo ya gharama za kambi na karo kwa ajili ya vijana wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 13 walioko shule ya Alliance Academy ya jijini Mwanza.
7. Huduma za kiutawala ikiwa ni pamoja na utunzaji viwanja na majengo, maji, umeme, ulinzi pamoja na mishahara na stahiki nyingine za wafanyakazi
8. Mwelekeo na mwitikio mzuri wa wadhamini uko kwenye hatari ya kupotea pindi mashindano na shughuli wanazozidhamini zitakapofubaa au kusimama kabisa.
9. Mkutano Mkuu wa kawaida wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) wa Mwaka 2015 uliopangwa kufanyika Tanga 19-20 Desemba 2015 sasa una hatihati ya kuweza kufanyika.
Hata hivyo, kwa kutambua umuhimu wa ulipaji kodi na wajibu wa Mamlaka ya Mapato katika kuhakikisha kodi inakusanywa kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Taifa,TFF ipo katika mawasiliano na TRA katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa suala hili ikiwa ni pamoja na kupitia upya mahesabu ili kujua wajibu halisi (net liability) wa TFF na namna ya kulipa au kulipwa kutegemea ulali wa mahesabu.
Hii si mara ya kwanza hili kujitokeza, lilijitokeza Oktoba 2012 na shilingi 157,407,968 iliyokuwa mgawo wa vilabu kuchukuliwa na TRA. Kufuatia tukio hilo, yalifanyika mazungumzo kati ya TFF na serikali ambamo ilikubaliwa kwamba fedha hizo zitarudishwa TFF na mpaka sasa TFF inafuatilia fedha hizo.
Kwa taarifa hii TFF inaomba utulivu kwa wanamichezo wote pamoja na ushirikiano wa karibu kutoka katika vyombo vyote husika ikiwemo TRA na wadau wengine ili jambo hili lipate ufumbuzi wa kudumu utakaoleta tija kwa serikali ya awamu ya tano ikiwa ni pamoja na kuongeza uwekezaji katika maendeleo ya mpira wa miguu na michezo kwa ujumla wake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli |

U-15 inarudia Mwanza katika ziara yake ya Afrika Mashariki |
Hata hivyo, kwa kutambua umuhimu wa ulipaji kodi na wajibu wa Mamlaka ya Mapato katika kuhakikisha kodi inakusanywa kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Taifa,TFF ipo katika mawasiliano na TRA katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa suala hili ikiwa ni pamoja na kupitia upya mahesabu ili kujua wajibu halisi (net liability) wa TFF na namna ya kulipa au kulipwa kutegemea ulali wa mahesabu.
Hii si mara ya kwanza hili kujitokeza, lilijitokeza Oktoba 2012 na shilingi 157,407,968 iliyokuwa mgawo wa vilabu kuchukuliwa na TRA. Kufuatia tukio hilo, yalifanyika mazungumzo kati ya TFF na serikali ambamo ilikubaliwa kwamba fedha hizo zitarudishwa TFF na mpaka sasa TFF inafuatilia fedha hizo.
Kwa taarifa hii TFF inaomba utulivu kwa wanamichezo wote pamoja na ushirikiano wa karibu kutoka katika vyombo vyote husika ikiwemo TRA na wadau wengine ili jambo hili lipate ufumbuzi wa kudumu utakaoleta tija kwa serikali ya awamu ya tano ikiwa ni pamoja na kuongeza uwekezaji katika maendeleo ya mpira wa miguu na michezo kwa ujumla wake.
0 comments:
Post a Comment