// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MNIGER WA YANGA SC SASA KUTUA DAR LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MNIGER WA YANGA SC SASA KUTUA DAR LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, December 08, 2015

    MNIGER WA YANGA SC SASA KUTUA DAR LEO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO wa kimataifa wa Niger, Issoufou Boubacar Garba (pichani kushoto) sasa anatarajiwa kuwasili leo usiku kwa majaribio ya wiki moja kabla ya kocha Hans van der Pluijm kutoa uamuzi.
    Awali, Garba ilikuwa awasili jana usiku, lakini imeelezwa alichelewa kuunganisha ndege mjini Addis Ababa, Ethiopia na kulazimika kulala hadi leo.
    Dirisha dogo la usajili la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara linafungwa Desemba 15 na kweli Mholanzi, Pluijm aliyempendekeza mchezaji huyo atakuwa na wiki moja tu ya kutoa majibu juu ya Mniger huyo aliyezaliwa Februari 2, mwaka 1990.
    Taarifa zinasema Garba kwa sasa anacheza kwao baada ya kuondoka Tunisia ambako alisajiliwa na klabu za Club Africain na ES Hammam-Sousse lakini akawa hapati nafasi ya kucheza, ingawa mwenyewe anadai kwa hila na visa si sababu ya uwezo.
    Popote katika wasifu wake, Garba anatambulishwa kama kiungo – lakini Yanga wanasema wanaleta mshambuliaji.
    Na huyu atakuwa mchezaji wa pili kuletwa na kocha Pluijm, baada ya awali kumleta beki Joseph Zuttah ambaye hata hivyo aliachwa baada ya mechi saba.
    Garba aliyezaliwa mji wa Niamey, mwenye urefu wa futi 5 na inchi 6, kisoka alianzia klabu ya AS FAN ya kwao mwaka 2010, kabla ya kuhamia Thailand ambako alichezea klabu za Muangthong United mwaka 2011 na Phuket.
    Mwaka 2012 alitua Club Africain ya Tunisia ambako hakucheza mechi hadi anahamishiwa 
    ES Hammam-Sousse ambako pia hakucheza.
    wasifu wake unaonyesha tangu ameondoka ES Hammam-Sousse hajapata timu nyingine, lakini uongozi wa Yanga SC umejiridhisha anachezea klabu bingwa ya kwao, AS Douanes.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MNIGER WA YANGA SC SASA KUTUA DAR LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top