// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MESSI ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA, BARCA NAYO YANG'ARA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MESSI ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA, BARCA NAYO YANG'ARA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, December 28, 2015

    MESSI ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA, BARCA NAYO YANG'ARA

    WASHINDI WA TUZO ZA GLOBE DUBAI 2015 


    Mchezaji Bora wa Mwaka 2015 - Lionel Messi
    Klabu Bora 2015 - Barcelona
    Rais Bora 2015 - Josep Maria Bartomeu
    Mvuto kwenye Vyombo vya Habari - Barcelona
    Tuzo ya Mchezaji Mkongwe- Frank Lampard
    Tuzo ya Mchezaji Mkongwe - Andrea Pirlo
    Wakala Bora 2015  - Jorge Mendes
    Kocha Bora 2015 -  Marc Wilmots
    Akademi Bora 2015 - Benfica
    Mchezaji Bora wa GCC 2015 - Yasir Al-Shahrani
    Refa Bora 2015 - Ravshan Irmatov 




    Lionel Messi (kushoto) akipokea tuzo ya Globe Soccer ya Mchezaji Bora wa Mwaka PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi ameng'ara katika usiku wa tuzo za Globe Soccer mjini Dubai baada ya kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka.
    Wababe wa La Liga, ambao walishinda mataji matatu msimu uliopita, wameshinda tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka, wakati Josep Maria Bartomeu ameshinda tuzo ya Rais Bora wa Mwaka.
    Mshambuliaji huyo wa Argentina, ambaye msimu huu amekuwa benchi kwa muda mrefu kutokakana na majeruhi, amefunga mabao 58 Barca na kufurahia ushindi wa kihistoria wa mataji matatu msimu uliopita.
    "Ni vizuri sana kupokea hizo tuzo, lakini wakati wote nasema timu inafanya haya mambo yawezekane,"amesema Messi. 
    Barcelona, ambayio pia imepewa tuzo ya Mvuto wa Kisoka kwenye Vyombo vya Habari, imeshinda mataji matano mwaka 2015, Ligi ya Hispania, Kombe lka Mfalme, Ligi ya Mabingwa, Super Cup ya Ulaya na Kombe la Dunia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MESSI ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA, BARCA NAYO YANG'ARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top