// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MBEYA CITY YASAJILI WANNE WAPYA, YAHAHA KUNASA MWINGINE KABLA YA KUIVAA MTIBWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MBEYA CITY YASAJILI WANNE WAPYA, YAHAHA KUNASA MWINGINE KABLA YA KUIVAA MTIBWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, December 09, 2015

    MBEYA CITY YASAJILI WANNE WAPYA, YAHAHA KUNASA MWINGINE KABLA YA KUIVAA MTIBWA

    Na Mwandishi Wetu, MBEYA
    KLABU ya Mbeya City FC imekamilisha usajili wa wachezaji wanne wapya, wakiwemo mabeki wa kati Tumba Sued Lui na Deo Julius ‘Msafa’.
    Meneja Usajili wa Mbeya City FC, Frank Michael Mfundo ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE mjini hapa kwamba, wachezaji wengine ni washambuliaji Abdallah Juma na Ditram Nchimbi.
    Mfundo amesema Mbeya City FC bado inashughulikia usajili wa mchezaji mwingine mpya, kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Desemba 15, mwaka huu.
    Tumba Lui Sued ni kati ya wachezaji wanne waliokamilisha usajili wao Mbeya City

     “Kwa mujibu wa mapendekezo ya mwalimu kwenye taarifa yake, tulikuwa na nafasi ya wachezaji watano, tayari tumekwishakamilisha wanne ambao ni Tumba Sued kutoka Coastal Union, Deo Julius kutoka Kagera Sugar, Abdallah Juma kutoka Toto African na Ditram Nchimbi aliyekuwa Majimaji FC,” amesema.
    Ameongeza kwamba wakati wowote watamtangaza mchezaji wa kukamilisha idadi ya wapya hao watano waliopendekezwa na mwalimu.
    Wakati huo huo: Kikosi cha Mbeya City FC leo kitakuwa Makambako kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Njombe Mji ya Njombe inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, ikiwa ni maandalizi ya mwishoni kabla ya mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar Jumamosi.
    Kikosi cha Mbeya City kimesafiri hadi Makambako kwa mchezo wa kirafiki
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY YASAJILI WANNE WAPYA, YAHAHA KUNASA MWINGINE KABLA YA KUIVAA MTIBWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top