Manji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Quality Group Limited, ameshinda tuzo, ambayo imeanzishwa wataalamu wa kuongoza kimataifa katika nyanja mbalimbali za kitaalamu na kuhakikisha uadilifu wa uteuzi bila uvunjwaji wa taratibu, kupitia jopo la maamuzi.
Na maamuzi hayo hufanywa kwa busara, na hivyo kuipa thamani tuzo hii ya kila mwaka katika uongozi.
Manji, amekuwa akijulikana kwa michango yake ya ubunifu katika Bara la Afrika hasa katika biashara, hana kikwazo kwenye kuwekeza kwa biashara nchini Tanzania ambayo, Quality Group inachangia asilimia 30% ya mapato nchini. VileVile kimataifa inaipa heshima ya kipekee kwenye biashara katika mabara manne.
Kutambuliwa na Umoja wa Mataifa hivi karibuni kwa ajili ya kusaidia katika mapambano ya kutokomeza ugonjwa wa Ebola katika Afrika ambapo zaidi ya dola za kimarekani 50,000,000 zilikusanywa (zaidi ya shilingi bilioni 100).
Akiizungumzia tuzo hiyo, Manji ameshukuru majaji wa kimataifa na Waziri ambaye alimkabidhi tuzo nchini Mauritius kwa mwakilishi wake.
"Kutambua ni mwanzo mzuri wa kufungua pazia kwa juhudi na utaalamu wa zaidi ya miaka 18 katika uongozi wa makampuni ya Quality Group ifikapo Juni, 2016,"amesema Manji na kuongeza;
"Napenda kukamilisha hoja yangu kutoka katika uongozi wetu wa biashara ya familia kwa changamoto mpya iliyopo mbele yangu, katika jamii na mafundisho juu ya ujasiriamali katika vyuo vikuu, wakati bado kijana mwenye nguvu ya kuwasiliana na vijana ambao wataweza kufanya mengi katika kuongeza wingi wa idadi ya watu wa Afrika,".
0 comments:
Post a Comment