Manchester United itamenyana na Midtjylland katika hatua ya 32 ya Europa League PICHA ZAIDI GONGA HAPA
TIMU ya Manchester United imepangwa na timu dhaifu, Midtjylland ya Denmark katika hatua ya 32 Bora ya Europa League.
Baada ya kutolewa na Wolfsburg katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, kikosi cha Louis van Gaal sasa kimeangukia Europa League.
Midtjylland ambayo ilianzishwa tu mwaka 1999 baada ya muungano wa klabu mbili, walitwaa taji lao la kwanza la ligi msimu uliopita.
Liverpool, ambayo kocha wake, Jurgen Klopp anahofia kukutana na timu yake ya zamani, Dortmund, itamenyana na timu nyingine ya Ujerumani, Augsburg.
Augsburg iliwashangaza wengi baada ya kumaliza juu ya Dortmund na Schalke katika Bundesliga msimu uliopita.
Tottenham ndiyo imekutana na shughuli pevu, baada ya kupewa have Fiorentina ndani ya mwaka mmoja baada ya kutolewa na timu hiyo ya Serie A kwenye mashindano hayo.
Valencia ya Hispania ya kocha Muingereza, Gary Neville imepangwa na Rapid Vienna na mechi za kwanza zinatarajiwa kuchezwa Februari 14 wakati marudiano yatakuwa wiki inayofuata.
0 comments:
Post a Comment