MATOKEO LIGI KUU YA ENGLAND LEO
Desemba 12, 2015
Bopurnemouth 2 – 1 Manchester United
Crystal Palace 1 - 0 Southampton
Sunderland 0 - 1 Watford
Manchester City 2 - 1 Swansea City
West Ham United 0 - 0 Stoke City
Norwich City 1 - 1 Everton
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Josh King akishangilia baada ya kuifungia Bournemouth dhidi ya timu yake hiyo ya zamani PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MANCHESTER United wamehitimisha wiki ya machungu, baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Vitality.
Mabao ya Bournemouth yamefungwa na Junior Stanislas dakika ya pili na Joshua King dakika ya 54, wakati la Man United limefungwa na Marouane Fellaini dakika ya 24.
Kipigo hicho kinakuja baada ya United kutolewa katoka hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katikati ya wiki, baada ya kufungwa mabao 3-2 na VfL Wolfsburg nchini Ujerumani.
Mechi nyingine za ligi hiyo leo, Crystal Palace imeshinda 1-0 dhidi ya Southampton, bao pekee la Yohan Cabaye dakika ya 38 Uwanja wa Selhurst Park, Watford imeshinda ugenini 1-0 dhidi ya Sunderland bao pekee la Odion Ighalo dakika ya nne Uwanja wa Light.
Manchester City imeshinda 2-1 dhidi ya Swansea City, mabao ya Wilfried Bony dakika ya 26 na Yaya Toure dakika ya 92, huku la wageni likifungwa na Bafetimbi Gomis dakika ya 90 Uwanja wa Etihad.
West Ham United imelazimishea sare ya 0-0 na Stoke City na Uwanja wa Boleyn Ground, wakati Norwich City imetoa sare ya 1-1 na Everton, bao lao likifungwa na Wes Hoolahan dakika ya 47, kabla ya Romelu Lukaku kuwasawazishia wageni dakika ya 15 Uwanja wa Carrow Road.

Mshambuliaji Romelu Lukaku akiwapigia saluti mashabiki wa Everton waliosafiri kwenda kuisapoti timu yao Uwanja wa Carrow Road baada ya kufunga katika mechi dhidi ya wenyeji Norwich, timu hizo zikitoka 1-1 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Mechi nyingine za ligi hiyo leo, Crystal Palace imeshinda 1-0 dhidi ya Southampton, bao pekee la Yohan Cabaye dakika ya 38 Uwanja wa Selhurst Park, Watford imeshinda ugenini 1-0 dhidi ya Sunderland bao pekee la Odion Ighalo dakika ya nne Uwanja wa Light.
Manchester City imeshinda 2-1 dhidi ya Swansea City, mabao ya Wilfried Bony dakika ya 26 na Yaya Toure dakika ya 92, huku la wageni likifungwa na Bafetimbi Gomis dakika ya 90 Uwanja wa Etihad.
West Ham United imelazimishea sare ya 0-0 na Stoke City na Uwanja wa Boleyn Ground, wakati Norwich City imetoa sare ya 1-1 na Everton, bao lao likifungwa na Wes Hoolahan dakika ya 47, kabla ya Romelu Lukaku kuwasawazishia wageni dakika ya 15 Uwanja wa Carrow Road.
0 comments:
Post a Comment