Leo Desemba 5, 2015
West Bromwich Albion 1-1 Tottenham Hotspur
Watford 2-0 Norwich City
Arsenal 3-1 Sunderland
Swansea City 0-3 Leicester City
Southampton 1-1 Aston Villa
Manchester United 0-0 West Ham United
Stoke City 2-0 Manchester City
LEICESTER City imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji Swansea City jioni ya leo Uwanja wa Liberty.
Shujaa wa Leicester leo alikuwa Riyad Mahrez aliyefunga mabao yote hayo dakika za tano, 22 na 67.
Matokeo hayo, yanaifanya Leicester ifikishe pointi 32 baada ya kucheza mechi 15 na inarejea kileleni baada ya Manchester City kufungwa 2-0 na Stoke City, mabao ya Marko Arnautovic dakika ya saba na 15 Uwanja wa Britannia.
Anthony Martial wa Manchester United, (kulia) akimtoka James Tomkins wa West Ham PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Manchester United nayo imelazimishwa sare ya 0-0 na West Ham United Uwanja wa Old Trafford leo katika mchezo ambao kila timu ilipoteza nafasi zaidi ya tatu za wazi za kufunga.
Arsenal imeshinda 3-1 dhidi ya Sunderland Uwanja wa Emirates, mabao yake yakifungwa na Joel Campbell dakika ya 33, Olivier Giroud dakika ya 63 akitoka kujifunga kuwapatia wageni bao dakika ya 45, kabla ya Aaron Ramsey kuwafungia The Gunners bao la tatu dakika ya 93.
West Bromwich Albion imelazimishwa sare ya 1-1 na Tottenham Hotspur Uwanja wa The Hawthorns bao lao likifungwa na James McClean dakika ya 39, baada ya Bamidele Alli kuanza kuwafungia Spurs dakika ya 15.
Watford imeichapa 2-0 Norwich City, mabao ya Troy Deeney kwa penalti dakika ya 30 na Odion Ighalo dakika ya 91 Uwanja wa Vicarage Road.
Southampton imetoka sare ya 1-1 na Aston Villa tena wenyeji hao wakilazimika kusawazisha kupitia kwa Oriol Romeu Vidal dakika ya 73, baada ya Joleon Lescott kuanza kuwafungia wageni dakika ya 44 Uwanja wa St. Mary's.
0 comments:
Post a Comment