KOCHA Muingereza wa Simba SC, Dylan Kerr amesema kwamba kikosi chake kipo tayari kukabiliana na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumamosi.
Simba SC iliyoweka kambi visiwani Zanzibar kwa takriban wiki mbili kujiandaa na mchezo huo, inatarajiwa kurejea kesho tayari kwa kipute cha Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
"Huu utakuwa ni mchezo wetu wa kwanza baada ya ligi kusimama kwa muda mfupi, ni mchezo ambao nategemea kuwa wa ushindani mkubwa, japokuwa kwa maandalizi ambayo kikosi changu kimeyafanya hadi sasa, mashabiki na wapenzi wa Simba waje kwa wingi siku hiyo Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuishangilia timu yao iweze kuushinda,"amesema Kerr.
"Nina imani kubwa sana ya kushinda katika mchezo huo, hivyo wapenzi wote wa Simba waje kwa wingi kuishangilia timu yao, najua Azam FC ni moja ya timu kubwa sana na itakuwa imejipanga vya kutosha kukabiliana nasi, ila siku ya Jumamosi nataka wachezaji wangu waonyeshe kuwa matokeo tuliyoyapata kwenye mechi yetu ya mwisho dhdi ya Majimaji ambapo tulishinda 6 -1 hayakuwa ya kubahatisha na hivyo tutaendeleza moto tuliokwisha uanza", aliongezea Kocha Kerr.

Kocha wa Simba SC, Muingereza Dylam Kerr (kushoto) amesema yuko tayari kwa mechi na Azam FC |
"Nina imani kubwa sana ya kushinda katika mchezo huo, hivyo wapenzi wote wa Simba waje kwa wingi kuishangilia timu yao, najua Azam FC ni moja ya timu kubwa sana na itakuwa imejipanga vya kutosha kukabiliana nasi, ila siku ya Jumamosi nataka wachezaji wangu waonyeshe kuwa matokeo tuliyoyapata kwenye mechi yetu ya mwisho dhdi ya Majimaji ambapo tulishinda 6 -1 hayakuwa ya kubahatisha na hivyo tutaendeleza moto tuliokwisha uanza", aliongezea Kocha Kerr.
0 comments:
Post a Comment