NAHODHA wa Chelsea, John Terry amerejea mazoezini na kumpa matumaini mapya kocha Jose Mourinho kuelekea mchezo muhimu wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumatano dhidi ya Porto.
Terry, ambaye anafikisha miaka 35 leo, amekaribishwa tena mazoezini sambamba na kiungo Mbrazil, Ramires katika mazoezi ya asubuhi leo Uwanja wa Cobham uliopo makao makuu ya The Blues.
Na anaweza kuingia moja kwa moja kwenye kikosi ambacho kinahitaji angalau pointi moja Uwanja wa Stamford Bridge kujihakikishia kuingia hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa.
Terry alifanya mazoezi mapema wiki iliyopita, lakini akaonekana hayuko fiti kiasi cha kutosha kucheza mechi dhidi ya Bournemouth Jumamosi PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Sasa mshambuliaji 'aliyechuja' Radamel Falcao ndiye anabaki mchezaji pekee anayekosekana Chelsea kutokana na mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United kuwa bado anasumbuliwa na maumivu ya misuli.
Terry amekosa mechi mbili zilizopita za Chelsea – Jumamosi wakifungwa 1-0 na Bournemouth na katika sare ya 0-0 na Tottenham – kutokana na kuumia kifundo cha mguu katika mchezo dhidi ya Maccabi Tel Aviv mwezi uliopita. Alifanya mazoezi mapema wiki iliyopita, lakini akaonekana hayuko tayari kuanza kucheza.
0 comments:
Post a Comment