MSHAMBULIAJI chipukizi, Farouk Miya ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu wa Ligi Kuu ya Azam Uganda kwa msimu wa 2014/2015.
Miya aliyezaliwa Novemba 26, mwaka 1997 anayechezea Vipers SC alikuwa Nahodha wa kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 23 cha Uganda na pia anachezea klabu bingwa ya Uganda, Vipers SC.
Amekuwa na mchango mkubwa, akipika mabao matano na kufunga 11, moja tu kwa kwa penalti na matatu kwa mipira ya adhabu ya moja kwa moja katika Ligi.
Miya ambaye amecheza Ligi Kuu ya Uganda kwa msimu mmoja na nusu tu, alikuwemo kwenye kikosi cha The Cranes kilichotwaa ubingwa wa CECAFA Challenge na tayari kwa sasa ni mchezaji tegemeo wa kikosi cha Mserbia Milutin Sredojevic 'Micho'.
Nyota huyo ambaye ni zao la Airtel Rising Stars, alifunga bao lake la kwanza The Cranes dhidi ya Shelisheli Uwanja wa Philip Omondi na kwa ujumla hadi sasa amecheza mechi 22 timu za taifa za U23 na ya wakubwa, Cranes na kuzifungia jumla ya mabao saba, likiwemo lile dhidi ya Nigeria katika ushindi wa 1-0 The Cranes ikiwafunga Super Eagles kwao.
Miya pia alifunga bao zuri dhidi ya Rwanda katika mechi za kufuzu za michauno ya U-23 Afrika na alikuwa Nahodha wa Uganda iliyotwaa taji la 14 la CECAFA Challenge nchini Ethiopia wiki iliyopita.
Farouk Miya akimkabidhi Kombe la CECAFA Challenge, Makamu wa Rais wa Uganda, Edward Kiwanuka Kiwanuka Ssekandi katika Ikulu ya Entebbe, huku Rais wa FUFA, Moses Magogo na kocha wa The Cranes, Milutin Sredojevic 'Micho' wakishuhidia

Farouk Miya ndiye mchezaji wa Ligi Kuu ya Azam Uganda 2014-2015 |

0 comments:
Post a Comment