// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HANS POPPE: HATUNA PRESHA NA KESSY, AMALIZIE MIEZI YAKE SITA, NDIYO TUFIKIRIE MKATABA MPYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HANS POPPE: HATUNA PRESHA NA KESSY, AMALIZIE MIEZI YAKE SITA, NDIYO TUFIKIRIE MKATABA MPYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, December 09, 2015

    HANS POPPE: HATUNA PRESHA NA KESSY, AMALIZIE MIEZI YAKE SITA, NDIYO TUFIKIRIE MKATABA MPYA

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba hawana papara ya kufanya mazungumzo ya Mkataba mpya na beki wao, Hassan Ramadhani Kessy.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo Dar es Salaam, Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Poppe amesema kwamba Kessy ana miezi zaidi ya kuitumikia Simba SC, hivyo hawana wasiwasi naye.
    “Mimi nashangaa hii presha inatokana na nini, huyu mchezaji ana miezi sita katika Mkataba wake wa sasa, amalize huu kwanza ndiyo tufikirie mazungumzo ya Mkataba mpya. Tunasikia amepata ofa ya Milioni 60 (Sh), aende akazungumze nao,”.
    Hans Poppe amesema hawana papara ya kufanya mazungumzo ya Mkataba mpya na Kessy

    “Ila sisi tutafanya naye mazungumzo wakati utakapofika, hatushinikizwi na magazeti kuzungumza naye, tunafanya mambo yetu kwa taratibu zetu,”amesema Poppe.
    Aidha, Mwenyekiti huyo wa Usajili wa Wekundu wa Msimbazi, amesema kwamba kwa sasa wapo katika mchakato wa kumuongeza Mkataba, kiungo Awadh Juma baada ya kumaliza aliokuwa anautumikia.
    Hassan Ramadhani Kessy amebakiza miezi sita katika Mkataba wake wa sasa

    Kessy aliyesajiliwa msimu uliopita kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, anatarajiwa kumaliza Mkataba wake Juni mwakani.
    Lakini kumekuwa na tetesi kwamba mchezaji huyo anatakiwa mahasimu, Yanga na Azam ambao wote wamewahi kukana kuwa na mpango huo – tena wakisema habari hizo zinavumishwa ili kuwatia presha Simba wampe Mkataba mpya mnono.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HANS POPPE: HATUNA PRESHA NA KESSY, AMALIZIE MIEZI YAKE SITA, NDIYO TUFIKIRIE MKATABA MPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top