Ibrahim Hajib (kulia) amefunga mabao mawili leo Simba SC ikishinda 5-2
KATIKA kujiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Desemba 12, Simba SC leo imeitandika mabao 5-2 timu ya Kimbunga FC ya Zanzibar katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na Ibrahim Hajib dakika ya 14 na 46, Danny Lyanga dakika ya 32, Nahodha Mussa hassan Mgosi dakika ya 38 na Haji Ugando. Baada ya mchezo huo, kocha wa Simba SC, Muingereza Dylan alisema kwamba mchezo ulikuwa mzuri na akawapongeza wachezaji wake. "Tunazitumia mechi hizi katika kuboresha kikosi chetu kuondoa sehemu ambazo timu yetu ilikuwa na changamoto mbalimbali lakini pia katika kuwajaribu wachezaji ambao wanendelea kufanya majaribio katika kikosi chetu,".
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment