// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); GIROUD AIPELEKA ARSENAL 16 BORA LIGI YA MABINGWA ULAYA, CHELSEA NAYO YAPETA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE GIROUD AIPELEKA ARSENAL 16 BORA LIGI YA MABINGWA ULAYA, CHELSEA NAYO YAPETA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, December 10, 2015

    GIROUD AIPELEKA ARSENAL 16 BORA LIGI YA MABINGWA ULAYA, CHELSEA NAYO YAPETA

    MATOKEO LIGI YA MABINGWA ULAYA
    Desemba 9, 2015  
    KAA Gent 2-1 Zenit St Petersburg
    Roma 0-0 BATE Borisov
    Dynamo Kyiv 1-0 Maccabi Tel Aviv
    Olympiakos 0-3 Arsenal
    Bayer 04 Leverkusen 1-1 Barcelona
    Valencia CF 0-2 Lyon
    Chelsea 2-0 FC Porto
    Dinamo Zagreb 0-2 FC Bayern Munich
    Giroud akishangilia baada ya kuifungia Arsenal mabao yote matatu PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    MSHAMBULIAJI Olivier Giroud usiku huu ameibuka shujaa baada ya kufunga mabao yote matatu, Arsenal ikishinda 3-0 ugenini dhidi ya wenyeji Olympiakos katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Georgios Karaiskakis, Giroud alifunga mabao hayo dakika za 29, 49 na 67 kwa penalti na kuifanya The Gunners kumaliza nafasi ya pili kwenye kundi hilo kwa kufikisha pointi tisa, nyuma ya Bayern Munich iliyomaliza na pointi 15.
    Lakini Arsenal inafuzu hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa kwa wastani wa mabao tu, kwani imefungana kwa pointi na Olympiakos iliyoishia nafasi ya tatu.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo, Bayern Munich imeshinda 2-0 ugenini dhidi ya Dinamo Zagreb, mabao yote akifunga Robert Lewandowski dakika ya 61 na 64 Uwanja wa Maksimir.


    Willian akishangilia baada ya kuifungia Chelsea katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Porto
     
    PICHA ZAIDI GONGA HAPA


    Chelsea nayo imekuwa timu ya tatu ya England kwenda 16 Bora ya michuano hiyo baada ya Manchester City na Arsenal, kufuatia ushindi wa mabao 2-0  dhidi ya FC Porto Uwanja wa Stamford Bridge katika mchezo wa Kundi G.
    Ivan Marcano Sierra alijifunga dakika ya 12 kuipatia The Blues bao la kwanza kabla ya Willian Borges Da Silva kufunga la pili dakika ya 52.
    Mchezo mwingine wa kudi hilo, Dynamo Kyiv imeshinda 1-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv, bao pekee la Denys Garmash dakika ya 16 Uwanja wa Olimpiki.
    Chelsea inamaliza kileleni mwa kundi hilo kwa pointi zake 13, ikifuatiwa Kyiv pointi 11, Porto pointi 10 na Maccabi ambayo haina pointi. 

    Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi akishangilia baada ya kuifungia timu yake  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    Katika mchezo wa Kundi E, Barcelona imelazimishwa sare ya 1-1 na Bayer 04 Leverkusen iliyoanza kupata bao kupitia kwa Javier Hernandez ‘Chicharito’ dakika ya 23, kabla ya  Lionel Messi kuwasawazishia mabingwa hao watetezi dakika ya 20 Uwanja wa BayArena.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo, Roma imetoka 0-0 na BATE Borisov Uwanja wa Olimpico. Barca inamaliza kileleni kwa pointi zake 14, ikifuatiwa na Roma pointi sita na sawa na Bayer 04 Leverkusen, wakati imeshika mkia kwa pointi zake tano.
    Valencia CF imefungwa 2-0 nyumbani na Lyon ua Ufaransa katika mchezo wa Kundi H.
    Katika mchezo huo uliofanyika Uwa ja wa Mestalla, mabao ya wageni yamefungwa na Maxwell Cornet dakika ya 37 Alexandre Lacazette dakika ya 76.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo, KAA Gent imeshinda 2-1 dhidi ya Zenit St Petersburg mabao yake yakifungwa na Laurent Depoitre dakika ya 18 na Danijel Milicevic dakika ya 78, huku la wageni likifungwa na Artem Dzyuba dakika ya 65 Uwanja wa Ghelamco Arena.
    Timu zilizofuzu 16 Bora ni Real Madrid, Paris Saint-Germain, VfL Wolfsburg, PSV, Atletico Madrid, Benfica, Manchester City, Juventus, Barcelona, Roma, FC Bayern Munich, Arsenal, Chelsea, Dynamo Kyiv, Zenit St Petersburg na KAA Gent.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GIROUD AIPELEKA ARSENAL 16 BORA LIGI YA MABINGWA ULAYA, CHELSEA NAYO YAPETA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top