// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MABAO MAWILI YAMNYIMA BOCCO UFUNGAJI BORA KOMBE LA CHALLENGE 2015 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MABAO MAWILI YAMNYIMA BOCCO UFUNGAJI BORA KOMBE LA CHALLENGE 2015 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, December 06, 2015

    MABAO MAWILI YAMNYIMA BOCCO UFUNGAJI BORA KOMBE LA CHALLENGE 2015

    MABAO mawili yamemnyima ufungaji bora mshambuliaji wa Tanzania, John Bocco (pichani) katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge.
    Katika michuano ya mwaka huu iliyofanyika nchini Ethiopia, Bocco maarufu kama ‘Adebayor’ amemaliza na mabao matatu, ingawa Tanzania ilitolewa katika Robo Fainali.
    Mwaka 2012 nchini Uganda, Bocco alifunga mabao matano na kuzidiwa bao moja na mfungaji bora wa mwaka huo, Brian Umony aliyefunga moja zaidi kwa penalti.
    Mshambuliaji wa Sudan iliyomaliza nafasi ya nne, Atahir Babikir amemaliza na mabao matano na kuwa mfungaji bora wa michuano ya mwaka huu.
    Bocco amefungana na Jacques Tuyisenge wa Rwanda, wakati Wakenya Jacob Keli na Michael Olunga wamemaliza na mabao mawili sawa na Chiukepo Msowoya wa Malawi, Elias Maguri, Simon Msuva wa Tanzania Bara, Farouk Miya, Ceasar Okhuti wa Uganda na Suleiman Kassim ‘Selembe’ wa Zanzibar.
    Beki wa Tanzania, Salum Mbonde pekee ndiye aliyeweka rekodi ya kujifunga katika michuano ya mwaka huu, akimfunga kipa wake katika mechi ya mwisho ya Kundi A dhidi ya Ethiopia.
    Waliofunga bao moja kila mmoja ni; 
    Walaaeldin Musa (Sudan), Jean Baptiste Mugiraneza (Rwanda), Panom Gathouch (Ethiopia), Frank Kalanda (Uganda), Khamis Mcha ‘Vialli’ (Zanzibar), Yussufu Habimana (Rwanda), Hegman Ngomirakiza (Rwanda), Faris Abdalla Mamoun (Sudan), Gerlad Phiri Jnr (Malawi), John Banda (Malawi), Mohammed Nasser (Ethiopia), Behailu Girma (Ethiopia), Elias Mamo (Ethiopia), Amissi Tambwe (Burundi), Said Ndemla (Tanzania Bara), Erisa Ssekisambu (Uganda), Dalitso Sailesi (Malawi), Bruno Martinez (Sudan Kusini), Dominic Abuyo (Sudan Kusini), James Joseph Saed (Sudan Kusini), Bruno Martinez (Sudan Kusini) na Didier Kavumbangu (Burundi).
    Uganda imetwaa taji la 14 la CECAFA Challenge baada ya kuifunga Rwanda bao 1-0 jana jioni katika mchezo wa fainali.
    Shukrani kwake mfungaji wa bao hilo pekee, Ceasar Okhuti aliyemalizia kwa kichwa krosi ya Dennis Okot kwa kumtungua Eric Ndayishimiye dakika ya 15.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MABAO MAWILI YAMNYIMA BOCCO UFUNGAJI BORA KOMBE LA CHALLENGE 2015 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top