// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA AFRICAN SPORTS MKWAKWANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA AFRICAN SPORTS MKWAKWANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, December 06, 2015

    AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA AFRICAN SPORTS MKWAKWANI

    AZAM FC imemaliza ziara ya siku tano mkoani Tanga kwa kutoka sare nyingine ya bao 1-1 dhidi ya African Sports katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Mkwakwani jana jioni mjini humio.
    Hiyo inakuwa sare ya pili kwa mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati, baada ya Alhamisi kutoka pia 1-1 na Mgambo JKT, bao la Azam FC likifungwa na Kipre Tchetche dakika 13 huku la Mgambo likipigwa na Fully Maganga dakika 87.
    Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall, alifanya mabadiliko mawili kikosini kwenye mchezo wa leo, akimwanzisha langoni kipa mpya mkongwe Ivo Mapunda badala ya Mwadini Ally na kumpumzisha beki Gardiel Michael na nafasi yake kuchukuliwa na Farid Maliki.
    Ivo Mapunda ameidakia mechi ya kwanza Azam FC jana ikitoa sare ya 1-1 na African Sports

    Kipa Ivo Mapunda kucheza mchezo huo kumemfanya awe amedaka mchezo wake kwanza ndani ya timu hiyo tokea asajiliwe kwenye usajili huu wa dirisha dogo.
    Azam FC iliuanza kwa kasi mchezo huo ikitaka kupata bao la mapema, lakini umakini wa safu ya ushambuliaji na umakini wa mabeki wa African Sports uliwanyima mabao.
    Dakika ya 36, almanusura mshambuliaji Kipre Tchetche, aipatie bao la uongozi Azam FC baada ya mpira safi wa adhabu ndogo alioupiga kwenye umbali wa takribani mita 30, kupanguliwa vema na kipa wa African Sports.
    Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza za mwamuzi Ibrahim Kidiwa kutoka Tanga, zinamalizika, timu zote zilienda vyumbani mapumziko milango ikiwa ni migumu.
    Kipindi cha pili kilianza kwa Azam FC kufanya mabadiliko kwa kuingia mabeki Said Morad ‘Mweda’ na David Mwantika wakichukua nafasi za Racine Diouf na Abdallah Kheri ‘Sebo’.
    Azam FC iliyokianza kwa kasi kipindi hicho, ilifanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya 46 kupitia kwa beki mkongwe wa timu hiyo, Erasto Nyoni, aliyepiga shuti baada ya kuinasa pasi ya kiungo mahiri Frank Domayo ‘Chumvi’.
    African Sports walicharuka baada ya kufungwa bao hilo na hatimaye wakasawazisha dakika ya 56 kwa njia ya mkwaju wa penalti uliopigwa na Rashid Ismaily.
    Baada ya African Sports kupata bao hilo, mpira huo ulionekana kuwa mkali sana kwa timu zote kushambuliana kwa zamu kwa kasi kubwa, huku Azam FC ikionekana kulifikia sana lango la wapinzani wao, ambao walikuwa wakitumia mashambulizi ya kushtukiza kupitia pembeni. 
    Hadi dakika 90 zinamalizika, timu hizo zilitoshana nguvu.
    Azam FC inarejea Dar es Salaam kuendelea maandalizi ya mchezo wake dhidi ya Simba SC Desemba 12, mwaka huu Uwanja wa Taifa.
    Kikosi cha Azam jana kilikuwa: Ivo Mapunda, Erasto Nyoni/Waziri Salum dk77, Farid Mussa/Gardiel Michael dk58, Abdallah Kheri/Said Mourad dk46, Pascal Wawa, Racine Diouf/David Mwantiuka dk46, Michael Bolou, Frank Domayo, Ramadhani Singano 'Messi', Kipre Tchetche na Shaaban Iddi/Khamis Mcha 'Vialli' dk46.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA AFRICAN SPORTS MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top