MATOKEO LIGI KUU YA ENGLAND LEO
Desemba 28, 2015
Manchester United 0-0 Chelsea
West Ham United 2-1 Southampton
Arsenal 2-0 Bournemouth
Everton 3-4 Stoke City
Watford 1-2 Tottenham Hotspur
Crystal Palace 0-0 Swansea City
West Bromwich 1-0 Newcastle United
Norwich City 2-0 Aston Villa
MECHI ZIJAZO…
Kesho Desemba 29, 2015
Leicester City v Manchester (Saa 4:45 usiku)
Desemba 30, 2015
Sunderland v Liverpool (Saa 4:45 usiku)
Mesut Ozil akishangilia baada ya kuifungia Arsenal bao la pili PICHA ZAIDI GONGA HAPA
ARSENAL imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya
Bournemouth jioni ya leo Uwanja wa Emirates, London.
Ushindi huo unawafanya Washika Bunduki hao wafikishe pointi 39, baada ya kucheza mechi 19, wakiizidi pointi moja tu Leicester City iliyocheza mechi 18.
Mabao ya timu ya Arsene Wenger leo yamefungwa na Gabriel Armando de Abreu dakika ya 27 na Mesut Ozil dakika ya 63.
Mchezo mwingine wa ligi hiyo leo, Manchester United imelazimishwa sare ya 0-0 na Chelsea Uwanja wa Old Trafford.
Nemanja Matic alipoteza nafasi ya wazi ya kufunga akiwa amebaki na David de Gea akapaisha PICHA ZAIDI GONGA HAPA
West Ham United imeshinda 2-1 nyumbani dhidi ya Southampton, mabao yake yakifungwa na Michail Antonio dakika ya 69 na Andy Carroll dakika ya 79, wakati Carl Jenkinson alijifunga dakika ya 13 Uwanja wa Boleyn Ground kuwapatia wageni bao la kuongoza.
Stoke City imeshinda ugenini 4-3 dhidi ya Everton Uwanja wa Goodison Park, mabao yake yakifungwa na Xherdan Shaqiri dakika ya 16 na 45, Jose Luis Mato Sanmartin dakika ya 80 na Marko Arnautovic kwa penalti dakika ya 91.
Mabao ya Everton yamefungwa na Romelu Lukaku dakika ya 22 na 64 na Gerard Deulofeu dakika ya 71. Tottenham Hotspur imeshinda ugenini 2-1 dhidi ya Watford mabao yake yakifungwa na Erik Lamela dakika ya 17 na Heung-Min Son dakika ya 89, wakati la wenyeji limefungwa na Odion Ighalo dakika ya 41 Uwanja wa Vicarage Road.
Nyota wa Tottenham Hotspur, Son Heung-min (kushoto) akishangilia baada ya kuifungia timu yake dakika ya 89 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Crystal Palace imelazimishwa sare ya 0-0 na Swansea City Uwanja wa Selhurst Park, wakati West Bromwich Albion imeshinda 1-0 dhidi ya Newcastle United bao pekee la Darren Fletcher dakika ya 78 Uwanja wa The Hawthorns na Norwich City imeshinda 2-0 dhidi ya Aston Villa, mabao ya Jonny Howson dakika ya 24 na Dieudonne Mbokani Bezua dakika ya 87 Uwanja wa Carrow Road.
Ligi Kuu inaendelea kesho, Leicester City wakiikaribisha Manchester City Uwanja wa King Power, wakati keshokutwa Sunderland watakuwa wenyeji wa Liverpool Uwanja wa Light.

0 comments:
Post a Comment