USHINDI wa 2-0 jana dhidi ya Afrika Kusini Uwanja wa Leopold Sedar Senghor mjini Dakar, ulitosha kuiwezesha Algeria kufuzu kwenye michuano ya Olimpiki kwa mara ya kwanza baada ya miaka 35.
‘Les Fennecs’ walishiriki Olimpiki ya Moscow, Urusi mwaka 1980 na washambuliaji Oussama Darfalou na Mohammed Benkhemassa walifunga kila kipindi kuipa timu yao tiketi ya Rio de Janeiro, Brazil mwakani sambamba na Nigeria.
Algeria itamenyana na Nigeria Jumamosi katika fainali ya michuano ya U23 yakiwa ni marudio ya mchezo wa makundi awali mwaka huu.
Katika Nusu Fainali ya kwanza, kiungo Etebo Oghenekaro aliifungia bao pekee Nigeria dhidi ya wenyeji Senegal kwa penalti na kuihakikishia tiketi ya Olimpiki.

Wachezaji wa Algeria wakifurahia ushindi wao jana dhidi ya Afrika Kusini |
0 comments:
Post a Comment