// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ZANZIBAR YAIBAMIZA KENYA 3-1 NA KUFUFUA MATUMAINI YA ROBO FAINALI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ZANZIBAR YAIBAMIZA KENYA 3-1 NA KUFUFUA MATUMAINI YA ROBO FAINALI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, November 27, 2015

    ZANZIBAR YAIBAMIZA KENYA 3-1 NA KUFUFUA MATUMAINI YA ROBO FAINALI

    MATOKEO NA RATIBA KOMBE LA CHALLENGE 2015
    Leo; Novemba 27, 2015
    Rwanda 3-0 Somalia
    Zanzibar 3-1 Kenya
    Sudan Kusini 2-0 Malawi
    Djibouti 0-4 Sudan
    Kesho; Novemba 28, 2015
    Uganda Vs Burundi 
    Tanzania Vs Ethiopia
    Zanzibar Heroes sasa yaweza kwenda Robo Fainali Challenge

    ZANZIBAR imeweka hai matumaini ya kwenda Robo Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kama mmoja wa washindi watatu bora, baada ya kuifunga Kenya mabao 3-1 jioni ya leo nchini Ethiopia.
    Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Suleiman Kassim ‘Selembe’ mawili na Khamis Mcha ‘Vialli’ moja, wakati bao la Kenya limefungwa na Jacob Keli.
    Rwanda imeifunga 3-0 Somalia, mabao ya Jacques  Tuyisenge, Yussufu Habimana na Hegman Ngomirakiza, wakati Sudan Kusini imeifunga 2-0 Malawi, mabao ya James Joseph Saed na Bruno Martinez.
    Sudan imeifunga Djibouti 4-0, huku gwiji wake, Athar El Tahir akipiga hat-trick ya kwanza ya mashindano na bao lingine likifungwa na Faris Abdalla Mamoun.  
    Michuano hiyo itaendelea kwa mechi mbili kesho, kati ya Uganda na Burundi na Tanzania Bara dhidi ya Ethiopia zikihitimisha hatua ya makundi kuelekea Robo Fainali.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZANZIBAR YAIBAMIZA KENYA 3-1 NA KUFUFUA MATUMAINI YA ROBO FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top