Na Ali Bakari, ZANZIBAR
CHAMA cha Mpira wa Miguu Zanzibar, ZFA kimepokea mualiko kutoka kwa Serikali ya kata ya Kilifi, iliyopo mji wa Malindi nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Beach Soccer yanayofanyika kila mwaka ndani mji huo.
Mualiko huu unaitaka timu ya taifa ya Mpira wa miguu wa Ufukweni, Zanzibar Sand Heroes kushiriki kwenye mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika tarehe 16-20 mwezi wa Disemba, 2015 kwenye fukwe za Buntwani, kata ya Kilifi, mji wa Malindi nchini Kenya.
ZFA kimepokea mualiko huo kwa moyo mmoja kikiamini kwamba ni mwendelezo mzuri wa kukuza ushirikiano na wenzao wa Kenya kwenye michezo lakini pia kuona kuwa Zanzibar Sand Heroes ni moja kati ya timu zitakazopeleka changamoto kwenye mashindano yao.
Chama hicho kinaamini hatua hiyo imekuja kufuatia ziara iliyofanywa mwezi Disemba mwaka jana na timu ya taifa ya Beach Soccer kutoka Uganda ‘Uganda Sand Cranes’ hapa nchini kuwa yenye mafanikio makubwa.
Lakini mbali na ziara hiyo, pia kuwepo kwa ligi ya Beach Soccer ambayo kwa asilimia kubwa sana kupitia vyombo vya habari kuitangaza vyema kulitoa msukumo mkubwa wa kutambuliwa na kufuatiliwa na nchi jirani.
Timu inatakiwa ilipe gharama za usajili (Registration fee) ambazo ni Shilingi Elfu tano za Kenya (Ksh. 5000) au Dola 50 za Kimarekani. Mbali na gharama hiyo ya usajili timu inatakiwa ijilipie yenyewe gharama za usafiri wa kwenda na kurudi nchini humo.
Kwa upande wa kamati ya mashindano ambayo inaoongozwa na Madam Melda Munyazi itatoa huduma za Chakula, Malazi, Usafiri na huduma nyengine zinazohusiana na mashindano hayo.
Kwa sasa chama hicho cha soka visiwani Zanzibar kinajipanga kuthibitisha ushiriki wao baada ya kukutana na kamati ya Beach Soccer ambayo imekubali kuupokea mualiko huo.
ZFA inaamini endapo Wazanzibar watashirikiana kwa pamoja timu za Zanzibar Sand Heroes na ile ya Zanzibar Heroes zitaleta ubingwa ndani ya nchi ufuatia mashindano yanayowakabili mbele yao.
kwa mara ya mwisho kikosi cha Zanzibar Sand Heroes kilishuka dimbani Disemba 7 mwaka jana kwenye fukwe za Bamboo maeneno ya Bububu nje kidogo ya mji wa Zanzibar kucheza na wageni wao kutoka Uganda 'Uganda Sand Cranes' kwenye pambano la kirafiki la kimataifa ambapo Zanzibar walikubali kichapo cha bao 5-4.
Kwa upande mwengine kikosi cha awali cha Zanzibar Heroes kilichotangazwa na kocha msaidizi Malale Hamsini Keya kinatarajiwa kuanza mazoezi rasmi hapo kesho majira ya saa 12:30 asubuhi uwanja wa Amaan chini ya kocha huyo akisaidiwa na kocha wa Makipa Saleh Machupa huku kocha mkuu wa kikosi hicho Hemed Suleiman 'Moroko' akiwa kwenye kambai ya Taifa Stars nchini afrika ya Kusini.

Kikosi cha Zanzibar Sand Heroes |

0 comments:
Post a Comment