KIPA Mbelgiji, Thibaut Nicolas Marc Courtois aliibukia klabu ya Bilzen V.V. ya kwao kama beki wa kushoto, kabla ya kuhamia Racing Genk mwaka 1999 akiwa ana umri wa miaka saba ambako huko ndipo alianzia kudaka.
Baada ya kufanya vizuri katika timu za vijana za Genk, Courtois alipandishwa timu ya wakubwa alipofikisha miaka 16 tu na siku 341, baada ya kuichezea kwa mara ya kwanza Aprili 17, mwaka 2009. Na alikuwa ana mchango mkubwa kwa Genk kutwaa taji la msimu wa 2010– 2011 wa Ligi Kuu ya Ubelgiji, kiasi cha kushinda tuzo ya Kipa Bora wa Mwaka na Mchezaji Bora wa Mwaka wa Genk, kutokana na kufungwa mabao 32 katika mechi 40, tena akisimama langoni mara 14 bila kuruhusu bao.
Kwa mafanikio hayo, Julai mwaka 2011 alinunuliwa na Chelsea ya England akisainishwa Mkataba wa miaka mitano.
Hata hivyo, Chelsea ilimpeleka kwa mkopo Atletico Madrid alikoanza kucheza mwaka 2013, kabla ya kumrejesha msimu huu akiwa ameiva kabisa na akipewa heshima ya mmoja wa makipa bora duniani.
Kocha Jose Mourinho akakubali kumuuza kipa mkongwe Petr Cech ili abaki na Mbelgiji huyo ambaye sasa ndiye kipa namba moja Stamford Bridge.
Makipa wapya wawili walisajiliwa Yanga SC mwanzoni mwa msimu, hao ni Benedicto Tinocco kutoka Kagera Sugar na Mudathir Khamis kutoka KMKM ya Zanzibar.
Tinocco alikuwa kipa wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 aliposajiliwa Yanga SC, wakati Mudathir alikuwa kipa wa Zanzibar na timu ya taifa, Taifa Stars.
Charles Boniface Mkwasa aliyekuwa kocha wa Yanga SC ambaye kwa sasa ni kocha wa Taifa Stars alianza kuachana na Mudathir timu ya taifa na kumchukua Said Mohammed wa Mtibwa Sugar badala yake.
Na juzi kimetajwa kikosi cha Zanzibar kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge nchini Ethiopia mwaka huu na huko pia Mudathir hayupo.
Uzuri ni kwamba, Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Hemed Morocco ndiye kocha Mkuu wa Zanzibar Heroes naye ameridhia Mudathir kuondolewa katika vikosi vyote.
Kwa upande wa Tinocco naye baada ya kuwa na mwanzo mzuri tangu alipoibuliwa kwenye mpango wa maboresho mwaka juzi, sasa ameanza kupotea.
Ndoto zake za kukua zaidi kisoka zinaanza kupotea – yaani kama alikuwa ana matarajio ya kupanda timu ya wakubwa, sasa yamepotea.
Na hiyo ni kwa sababu gani? Tangu wawili hao kusajiliwa Yanga SC Julai mwaka huu wamekwenda kuwa wa kufanya mazoezi bila ya kucheza mechi.
Mudathir amedaka mechi moja tu ya kirafiki kwa dakika 45 mjini Mbeya dhidi ya Kemondo, wakati Tinocco hajacheza mechi Yanga SC.
Na si kwamba wanaonewa, bali hawafurukuti mbele ya makipa waliopo, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’.
Lakini kama wangebaki katika klabu zao wangeendelea kucheza na kuweka hai ndoto zao za mafanikio zaidi kisoka, tena huku wakizisaidia na klabu zao.
Huwezi kuwalaumu wachezaji kwa kusaini Yanga SC kwa sababu wazi wamevutiwa na klabu kubwa na ofa nzuri ya dau la usajili.
Lakini huwezi kukwepa kuwalaumu Yanga SC, wanaonekana ni klabu ambayo inakosa mipango kidogo ya kuendeleza vipaji.
Makipa hawa wawili walikamilisha usajili wao Yanga SC mapema tu kabla ya dirisha kufungwa ina maana uongozi ulijua utaingia katika msimu mpya ukiwa na makipa wanne; Barthez, Dida, Muda na Tinocco.
Barthez ndiye ‘Yanga One’ na msaidizi wake ni Dida- ukiwa na makipa hawa wawili tu pekee ni lango lako liko salama sana.
Wote wana nidhamu ya ndani na nje ya Uwanja ni nadra kutokea wakaadhibiwa kwa kadi, labda ziwe za njano na tena kwa sababu kuchelewesha muda tu. Ukiona Barthez au Dida mmoja wapo hayupo kazini ni kwa sababu ya majeruhi tu.
Baada ya kuwa na makipa hawa wa zamani wa Simba SC, Barthez na Dida – Yanga SC ilihitaji labda kipa mmoja wa ziada kwa kuhofia ikitokea mmojawao akaumia au kusimamishwa, wabaki wawili.
Lakini matokeo yake Yanga SC wamejiruhusu kuingia msimu mpya na makipa wanne, ambao kati yao wawili hawatumiki kabisa.
Hata zikija hoja za kurejeshwa Kombe la TFF (zamani FAT), bado hiyo itakuwa nafasi nzuri kwa kipa wa pili na wa tatu nao kulinda vipaji vyao.
Tazama sasa Yanga SC inaua vipaji vya makipa hawa ambao walishakuwa kwenye mwelekeo mzuri kisoka na mwishowe itakuja kuwaacha tu, tena kihalali kabisa.
Kwa sababu hawachezi na wakimaliza mikataba yao ya sasa ndiyo ‘bye bye’ na watasajiliwa wengine, nao wataua vipaji vyao kisha wataachwa. Historia itaendelea tena na tena na tena.
Mei 6, mwaka 2012 katika mchezo dhidi ya watani wa jadi, Simba SC Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kipa Yaw Berko raia wa Ghana alishindwa kuendelea na mchezo baada ya Yanga kufungwa 1-0 kipindi cha kwanza.
Akaingia kipa wa tatu, Said Mohammed ambaye alifungwa mabao manne zaidi, matatu kwa penalti na baada ya dakika 90, Yanga ikalala 5-0.
Zaidi ya Berko na Said, kipa mwingine aliyekuwa Yanga SC alikuwa Shaaban Hassan Kado ambaye alikuwa namba mbili.
Ikumbukwe Said Mohammd alisajiliwa kutoka Majimaji mwaka 2010 akiwa katika kiwango kizuri kiubora kiasi cha kuitwa Taifa Stars.
Ikumbukwe pia, Yanga SC ilimsajili kipa huyo baada ya kuzizidi kete Azam FC na Simba SC zilizokuwa zinamuwania pia. Lakini baada ya msimu wa 2011-2012, Said aliachwa na kwa bahati nzuri akaenda Mtibwa Sugar alipofanikiwa kufufua kiwango chake na sasa amerudi hadi Taifa Stars.
Yanga SC wanapata somo gani kwa sasa baada ya makosa waliyofanya kwa Said labda na Kado pia na hata wachezaji wengine iliyowasajili wakati haina nafasi ya kuwatumia?.
African Sports wangefurahi kuwa na kipa mzoefu na wa kiwango cha Mudathir Khamis ‘anayechoma mahindi’ Yanga SC.
Hata Kagera wangefurahi kubaki na Tinocco na hakuna ubaya wowote kama Yanga SC ingewatoa huko kwa mkopo ili waendelee kucheza.
Na zaidi hiyo ingekuwa faida kwa Yanga SC kwa sababu kule wangeendelea kucheza na kukuza viwango vyao, kuliko ilivyo sasa wanaua viwango vyao.
Chelsea ingefanya kama Yanga kwa Courtois kwamba baada ya kumsajili ‘ikamchomeshe mahindi’, leo angekuwa amekwishapotea siku nyingi. Lakini sasa wanavuna matunda ya uwekezaji wao.
Lakini hayo si mawazo yao na ndiyo maana watu wengine wanasema Yanga inaua vipaji vya wachezaji – watakataa vipi kama mambo yenyewe ndiyo haya?

0 comments:
Post a Comment