Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
SI umesikia ‘uvumi’ kwamba eti Yanga SC wanamtaka beki wa Simba SC, Hassan Ramadhani Kessy? Basi Yanga Yanga SC wamewatoa hofu mahasimu wao, Simba SC kwa kuwaambia; “Hatuna kabisa mpango wa kusajili mchezaji wa Simba SC, haswa haswa hawa wa ndani,”.
Hayo ni maneno ya Katibu Mkuu wa Yanga SC, Dk Jonas Tiboroha akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE asubuhi ya leo mjini Dar es Salaam.
Na Tiboroha amesema anachoona kwa sasa juu ya kuvumishwa kwa habari za Kessy kutakiwa Yanga SC ni kumtafutia umaarufu mchezaji huyo, ili aongezewe Mkataba na klabu yake.
“Hapa watu wanataka kumpa kiki (umaarufu) huyu mtoto ili aongezewe Mkataba Simba, lakini sisi hatuna time (muda) naye kabisa,”amesema Tiboroha.
Katibu huyo amesema kwamba mapema mwaka huu uongozi wa Yanga SC ulifikia makubaliano ya kutosajili mchezaji yeyote mzalendo wa Simba SC, labda wa kigeni tu.
Na akasema kama si azimio hilo, wangeweza kumsajili kiungo Said Ndemla kabla ya kusaini Mkataba mpya Simba SC Agosti mwaka huu.
Lakini kwa ujumla Tiboroha amesema Yanga SC haina mpango wa kusajili mchezaji katika kipindi hiki cha dirisha dogo, labda itokee wauze mchezaji.
“Hatuna mahitaji ya kusajili. Labda itokee tumeuza mchezaji, ndiyo tutasajili kuziba pengo lake,” amesema Tiborobha.
Ameongeza kwamba Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mholanzi Hans van der Pluijm amewasilisha programu yake inayoanza leo, ambayo ndani yake amehitaji tu kambi ya mazoezi na mechi za kujipima nguvu dhidi ya timu za nje.
Yanga SC imeanza mazoezi leo Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini, Dar es Salaam baada ya mapumziko ya wiki mbili kufuatia kusimama kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kupisha maandalizi ya timu ya taifa, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo dhidi ya Algeria Jumamosi na Jumanne kufuzu Kombe la Dunia.
Na katika mazoezi hayo, Yanga SC inawakosa wachezaji wake waliopo timu ya taifa, kipa Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, viungo Salum Telela na washambuliaji Simon Msuva na Malimi Busungu.
Yanga SC pia inawakosa wachezaji wake wa kigeni wawili, waliokwenda kuzitumikia timu zao za taifa katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi, ambao ni beki Vincent Bossou wa Togo, kiungo Haruna Niyonzma wa Rwanda na mshambuliaji Amissi Tambwe wa Burundi.

Yanga SC imesema haina mpango na Hassan Kessy kama inavyovumishwa |

0 comments:
Post a Comment