Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
WASHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu wanatarajiwa kuondoka leo Lubumbashi kwenda Johannesburg, Afrika Kusini kujiunga na kambi ya timu ya taifa.
Taifa Stars imeweka kambi Johannesburg, Afrika Kusini kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia katikati ya mwezi huu – na Samatta na Ulimwengu wanakwenda kambini siku moja baada ya kuisaidia klabu yao, TP Mazembe kutwaa ubingwa wa Afrika.
Samatta alifunga bao moja na kuseti moja, TP Mazembe ikitimiza dhamira ya kutwaa ubingwa wa Afrika baada ya kuifunga 2-0 USM Alger ya Algeria.
Mchezo huo wa marudiano wa fainali ya Ligi ya Mabingwa uliofanyika Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, wenyeji walipata mabao yote kipindi cha pili.
Na Mazembe inatwaa taji la tano la Ligi ya Mabingwa kwa ushindi wa jumla wa 4-1, baada ya awali kushinda 2-1 mjini Algiers Jumapili iliyopita.
Samatta jana aliwekewa ulinzi mkali na wachezaji wa USM hadi akalazimika kusubiri kufunga bao lake la saba katika michuano ya mwaka huu kwa penalti dakika ya 75, baada ya Rogger Asale kuangushwa.
Samatta naye akamsetia pasi nzuri Assale kufunga bao la pili katika dakika za majeruhi baada ya kutimia dakika 90 za kawaida za mchezo.
Matokeo hayo yanamfanya Samatta pia awe mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa msimu huu, baada ya kufikisha mabao saba, sawa na Bakri Al-Madina wa El-Merreikh ya Sudan.
Hii maana yake huu unakuwa mwaka wa pili mfululizo, Tanzania inatoa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa, baada ya mwaka jana Mrisho Khalfan Ngassa kuongoza pia akiwa na klabu ya Yanga SC, kabla ya kuhamia Free State Stars ya Afrika Kusini msimu huu.
Ngassa alifunga mabao sita sawa na El Hedi Belameiri wa Setif, Haythem Jouini wa Esperance na Ndombe Mubele aliyekuwa AS Vita ya DRC, sasa Al Ahly.
Taifa Stars itaikaribisha Algeria Jumamosi ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya kurudiana mjini Algies Novemba 17 na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi kuwania tiketi ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

Mbwana Samatta (kulia) akikimbia kushangilia na Mtanzania mwenzake, Thomas Ulimwengu baada ya kufunga bao la kwanza |

0 comments:
Post a Comment