Na Salum Vuai, ZANZIBAR
TANGU katikati ya mwaka jana, soka la Zanzibar limekuwa likipita katika kipindi kigumu cha kudorora kutokana na kukumbwa na migogoro ya kikatiba na kimadaraka.
Kufunguliwa mashtaka kwa viongozi wa juu wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA)na kiongozi mwenzao mmoja, ni tukio lililozidi kukiongezea saratani chama hicho.
Bila shaka, hayo na mengine ni mambo yanayowapa majonzi wanachama wa ZFA, yaani klabu za madaraja mbalimbali pamoja na mashabiki, kwa kuwa wamekosa burudani ya soka waliyoizoea, iliyotoweka baada ya kuzuiwa ligi hizo kufanyika.
Hali hiyo ikaongezewa nguvu baada ya mahakama kuu ya Zanzibar kuamuru kuondolewa madarakani kwa viongozi wa chama hicho kwa madai kwamba wana kesi ya kujibu.
Hatua hiyo iliishia kwa agizo la kuundwa kamati ya muda kusimamia shughuli za chama hicho kwa lengo la kurejesha utulivu na mpira wa miguu viwanjani.
Ni jambo la kufurahisha kwamba, ujio wa kamati hiyo umeonesha mwanga wa matumaini ya hali ya soka la Zanzibar kurudi kama ilivyokuwa awali kabla ya suitafahamu kuibuka.
Hatua ya kamati hiyo kukutana na uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mwanzoni mwa wiki hii, na pia kuwashirikisha viongozi wa chama hicho waliokuwa wameenguliwa na mahakama, ni ya kupongezwa na wote wenye nia njema na soka la Zanzibar.
Aidha, ninapenda kuchukua nafasi hii kuunga mkono maazimio yote yaliyopitishwa na kukubaliwa kwenye kikao hicho, ambayo ni dhahiri yanalenga kusafisha hali ya hewa na kurejesha furaha kwa wadau wa mpira wa miguu nchini.
Katika hili, ni lazima wale wanaojiita wadau wa soka washushe munkari wao na kuipa ushirikiano kamati na viongozi hao wa ZFA ambao awali waliwekwa kando, kama kweli wanataka mpira Zanzibar uendelee.
Kwani nia ya wote si kustawisha soka letu?
Kama hilo ndio lengo, hakuna sababu ya kuendelea kuvutana na kugombea fito wakati sote tunajenga nyumba moja.
Kwa kuwa kila jambo linaongozwa na sheria na kanuni zilizowekwa, kwa mujibu wa katiba za taasisi husika, lazima mambo yaendeshwe kwa kufuata mkondo huo.
Yumkini katiba ya ZFA ina kasoro zinazoleta utata, lakini hilo haliwezi kurekebishwa kama kila mmoja atajiona ndiye mwenye haki na wengine hawana lao.
Kama kweli tunataka kupata ufumbuzi wa kudumu wa matatizo haya yanayokitafuna chama, ni vyema kuunganisha nguvu na kuweka kando tofauti zinazotugawa katika azma ya kustawisha soka letu.
Fikra za kila mmoja zinafaa kupewa nafasi ya kusikika na kufanyiwa tathmini ili kuchukua zile tutazokubaliana kwamba zinaweza kuleta tija, lakini hilo litekelezwe kwa vikao vya pamoja vyenye lengo la kuweka mambo sawa.
Panapokuwa na hitilafu, kama wapo wanaojitolea kuleta suluhu, si jambo la busara watu wengine wakae vipembeni kuzibeza juhudi zinazochukuliwa na wenzao.
Tangu ilipoundwa kamati ya muda kwa ajili ya kurejesha utulivu ndani ya ZFA, mara kadhaa ninaposoma mitandao ya kijamii, nimeshuhudia maoni tofauti yanayotolewa yenye kuibeza kamati hiyo.
Baadhi ya watu wamekuwa wakitumia mitandao hiyo hasa 'facebook', kuiponda kamati hiyo na kuandika ujumbe wenye kukejeli kila hatua inayochukuliwa.
Inashangaza watu hawa walifurahi hata pale Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilipoiandikia barua ya indhari ZFA kwamba kama mzozo wao hautapatiwa dawa na kesi zilizoko mahakamani kuondolewa, iko hatarini kufungiwa.
Badala ya kuhuzunika, wapo miongoni mwa Wazanzibari, na ajabu zaidi baadhi yao ni waandishi wa habari, ambao walikunwa na onyo hilo na ninaamini nyoyoni mwao wakiombea litokee.
Yaonesha hawa walikuwa wamemili upande mmoja kati ya wagombanao, na kusahau kwamba wakiwa waandishi wa habari, walipaswa kufanya wajibu wa kushauri ili zogo hili lifikie ukomo na mpira wetu urudi.
Kunapokuwa na matatizo ya uendeshaji katika vyama vya michezo, si vibaya waandishi wa habari kuandika na kutangaza kwa lengo la kuujuulisha umma nini kinaendelea.
Lakini inakuwa aibu kwao kujiegemeza upande mmoja na kutumia kalamu na vipaza sauti vyao kuurushia madongo upande mmoja wa wazozanao.
Penye migogoro, daima waandishi wa habari wanatakiwa wakae kati, na wasiwe mashabiki wa upande wowote, ingawa hilo halipaswi kuwazuia kuandika kila kitu kwa ukweli na kwa mujibu kilivyo, lengo ikiwa ni kuleta suluhu.
Kuwepo kwa mitandao ya kijamii, kusiwafanye waandishi wakiuke uhuru walionao na kuweka kando taaluma na maadili yanayoongoza kazi zao.
Wala pale baadhi wanapoganda kwenye ukweli, kuacha nidhamu ya woga na kuamua kuweka mambo hadharani kwa manufaa ya umma wanaoutumikia, watu wengine wakiwemo waandishi wenzao hawapaswi kuwabomoa kupitia mitandao kama 'facebook' 'twitter', 'WhatsApp' na mingine.
Sote tuna wajibu mkubwa wa kulibeba hili kwa pamoja kwani ni letu sote, wala si la ZFA, BTMZ au kamati ya muda pekee.
Kama ni ujenzi, basi kila mmoja anapaswa kuwemo katika mstari tukipasiana matofali mkono kwa mkono hadi jengo tunalolijenga litakaposimama.
Umefika wakati sasa tumuue bundi aliyehamia katika paa la soka letu ili kuviamsha viwanja vyetu vilivyolala usingizi wa pono kwa kukimbiwa na ligi zetu.
(Mwandishi wa makala haya anapatikana kwa nambari +255 777 865050 na +255 714 425556 au barua pepe salumss@yahoo.co.uk)

Kikosi cha Mafunzo ya Zanzibar, moja ya waathirika wa mgogoro wa kisoka visiwani humo |

0 comments:
Post a Comment