Na Philipo Chimi, MWANZA
KLABU Toto Africans ya Mwanza imeandaa mkutano maalum kwa wanachama wake kwa ajili ya kufanya harambee kuchangia timu hiyo iweze kushiriki vyema Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Godwine Aiko amesema kwamba wameandaa mkutano huo kufuatia hali mbaya ya kiuchumi inayoikabili timu.
Amesema timu inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji utatuzi wa haraka ili kunusuru mwendo wake mbovu katika Ligi Kuu.
“Tumeandaa mkutano huo ambao utafanyika siku ya Novemba 22 kwa ajili ya kufanya mipango kuona namna gani timu inapata fedha,” amesema na kuongeza.
“Kwa sasa kuna mipango tumefanya ya kuomba makampuni yatusaidie na tumepata kampuni moja, ila bado haijatoa jibu sahihi. Mbali na hilo, pia tutajadili mwenedo wa timu kwa kupokea taarifa kutoka benchi la ufundi,”aliongeza Aiko.
Timu hiyo ya Mtaa wa Kishamapanda, Mwanza inakabiliwa na ukata wa fedha kiasi cha kushindwa kulipa hata mishahara ya wachezaji, hali iliyosababisha Kocha Mkuu, Martin Grelics raia wa Ugeruman ang’atuke.

Wachezaji wa Toto Africans wakiwa na bango la kumuaga kocha wao Martin mwezi uliopita Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam |
“Tumeandaa mkutano huo ambao utafanyika siku ya Novemba 22 kwa ajili ya kufanya mipango kuona namna gani timu inapata fedha,” amesema na kuongeza.
“Kwa sasa kuna mipango tumefanya ya kuomba makampuni yatusaidie na tumepata kampuni moja, ila bado haijatoa jibu sahihi. Mbali na hilo, pia tutajadili mwenedo wa timu kwa kupokea taarifa kutoka benchi la ufundi,”aliongeza Aiko.
Timu hiyo ya Mtaa wa Kishamapanda, Mwanza inakabiliwa na ukata wa fedha kiasi cha kushindwa kulipa hata mishahara ya wachezaji, hali iliyosababisha Kocha Mkuu, Martin Grelics raia wa Ugeruman ang’atuke.
0 comments:
Post a Comment