// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TAIFA STARS YA BAADAYE YAKABIDHIWA BENDERA KWA ZIARA YA AFRIKA MASHARIKI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TAIFA STARS YA BAADAYE YAKABIDHIWA BENDERA KWA ZIARA YA AFRIKA MASHARIKI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, November 29, 2015

    TAIFA STARS YA BAADAYE YAKABIDHIWA BENDERA KWA ZIARA YA AFRIKA MASHARIKI

    TIMU ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) leo hii imekabidhiwa bendera ya Taifa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel katika hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam.
    Akiongea wakati wa kukabidhi bendera kwa timu hiyo ya vijana, Ole Gabriel amewashukuru TFF kwa kuwekeza katika soka la vijana, na kusema mafaniko yote yanandaliwa chini, hivyo analipongeza Shirikisho kwa kuamua kuwalea na kuwaendeleza vijana hawa wenye vipaji kwa manufaa ya taifa ya baadae.

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akiwakabidhi bendera U15 

    Ole Gabriel amewataka vijana waliochaguiwa katika kikosi hicho, kuitumia nafasi hiyo adimu ipasavyo kuwawakilisha watanzania, kujituma katika mafunzo wanayopewa na waalimu wao, nidhamu ndani na nje ya uwanja na kuonyesha uzalendo wao wanapoiperesuha bendera ya Taifa.
    Kikosi hicho cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 kinatarajiwa kuondoka kesho alfajiri (Jumatatu) kuelekea jijini Mwanza kwa mchezo wa kirafiki na kombaini ya mkoa wa Mwanza (U17), kisha kuelekea mkoani Kigoma kwa michezo miwili ya kirafiki dhidi ya kombaini ya mkoa wa Kigoma (U17) na timu ya Taifa ya Burundi (U17).
    Baada ya michezo ya mkoani Kigoma, U15 itaelekea Kigali Rwanda kwa michezo na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, kisha Jinja kucheza na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Uganda, Nairobi itacheza na timu ya taifa ya Kenya (U17) na kumalizia jijini Arusha kwa kucheza na kombaini ya mkoa wa huo (U17).
    Timu inatarajiwa kurejea jijini Dar ess alaam Disemba 24 baada ya kuwa imecheza michezo kumi ya kirafiki, mechi hizo zitampataia nafasi kocha mkuu Sebastiani Mkomwa kuona maendeleo ya vijana wake, wakiajiandaa kucheza michezo ya kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika U17 mwaka 2017 nchini Madagascar.

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akifunga programu ya Live Your Goal

    Wakati huo huo: Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel leo amefunga program ya Live Your Goal iliyoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
    Ole Gabriel amewashukuru vijana waliojitokeza kushiriki katika program hiyo na kuwaomba wazazi kuwarushu watoto wa kike kujtokeza na kushiriki katika program hiyo ya kuhamasisha wanawake kucheza mpira wa miguu.
    Live Your Goal ni program inayoendeshwa na TFF kwa msaada kutoka FIFA yenye lengo la kuwahamasisha watoto wa kike, na wasichana kujitokeza kuucheza na kuupenda mpira wa miguu.
    Programu hii iliyomalizika leo imejumuisha vilabu sita vya wanawake, kutoka wilaya za Ilala, Kinodoni na Temeke, shule za msingi sita kutoka jijini Dar es salaam ambapo washiriki walikua wanafunzi wenye umri kaunzia miaka 8 na kuendelea, na ikifanyika kwa mara ya pili baada ya awalia mwezi Juni mwaka huu mkoani Geita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA STARS YA BAADAYE YAKABIDHIWA BENDERA KWA ZIARA YA AFRIKA MASHARIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top