Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
ABAJALO FC ya Sinza imeanza vyema michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Azam Sports HD Federation Cup baada ya kuifunga Transit Camp mabao 5-1 jioni ya leo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Shujaa wa Abajalo leo alikuwa ni mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Ramadhani Kipalamoto aliyefunga mabao manne peke yake.
Kipalamoto alifunga mabao yake katika dakika za
tatu, 12, 43 na 60 wakati bao lingine la Abajalo limefungwa na Soud Mohammed dakika ya 40.
Venus Mgini aliifungia bao la kufutia machozi Transit Camp dakika ya 84 ingawa halikuinusuru timu hiyo ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuaga mashindano hayo.
Mchezo huo ulihudhuriwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi pamoja na Mtendaji Mkuu wa Azam TV, wadhamini wa mashindano, Muingereza Rhys Torrington ambao wote walipiga penalti kuashiria ufunguzi wake.
Mchezo mwingine wa michuano hiyo leo, Pamba FC imeifunga Bulyanhulu FC 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Kikosi cha Abajalao FC kilikuwa; William Ismail, Mussa Olowa, Godfrey Sabas, Roland Narsis, Dunni Frank, Abdallah Kapalama/Ramadhani Amour dk57, Soud Mohammed/Suleiman Ibrahim dk71, Kelvin Nashon, Ramadhani Kipalamoto, Lameck Dayton na Jamal Mbelwa/Waziri Omar dk57.
Trans Camp; Omary Mohammed, Agaton Oscar, Abubakar Iddi, Godfrey Stefano/Thomas Chindeka dk48, Omary Hassan, Athumani Kisatu, Buhaga Wallya, Daud Igge/Kombo Mussa dk39, Hussein Nyamandulu/Mohammed Omary dk55, Venus Mgini na Prosper Pius.

Ramadhani Kipalamoto (kushoto) akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao la pili kati ya manne katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Transit Camo leo Uwanja wa Karume |
Ramadhani Kipalamoto (kushoto) akimtoka beki wa Transit Camp |
Rais wa TFF, Jamal Malinzi akisalimiana na marefa kabla ya mchezo |
Venus Mgini aliifungia bao la kufutia machozi Transit Camp dakika ya 84 ingawa halikuinusuru timu hiyo ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuaga mashindano hayo.
Mchezo huo ulihudhuriwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi pamoja na Mtendaji Mkuu wa Azam TV, wadhamini wa mashindano, Muingereza Rhys Torrington ambao wote walipiga penalti kuashiria ufunguzi wake.
Mchezo mwingine wa michuano hiyo leo, Pamba FC imeifunga Bulyanhulu FC 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Kikosi cha Abajalao FC kilikuwa; William Ismail, Mussa Olowa, Godfrey Sabas, Roland Narsis, Dunni Frank, Abdallah Kapalama/Ramadhani Amour dk57, Soud Mohammed/Suleiman Ibrahim dk71, Kelvin Nashon, Ramadhani Kipalamoto, Lameck Dayton na Jamal Mbelwa/Waziri Omar dk57.
Trans Camp; Omary Mohammed, Agaton Oscar, Abubakar Iddi, Godfrey Stefano/Thomas Chindeka dk48, Omary Hassan, Athumani Kisatu, Buhaga Wallya, Daud Igge/Kombo Mussa dk39, Hussein Nyamandulu/Mohammed Omary dk55, Venus Mgini na Prosper Pius.
0 comments:
Post a Comment