Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inaondoka Dar es Salaam Saa 4:00 asubuhi ya leo kwenda Johannersburg, Afrika Kusini kuweka kambi ya siku 10 kujiandaa na mchezo dhidi ya Algeria katikati ya mwezi ujao.
Taifa Stars itamenyana na Algeria katika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia 2018 Urusi, baada ya kuitoa Malawi katika hatua ya kwanza.
Na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limebadili mpango wa kambi ya Oman kutokana na taratibu ngumu za kupata viza, badala yake timu inakwenda Afrika Kusini.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ataondoka na wachezaji wote 24 kati ya 28 aliowaita wiki iliyopita katika kikosi chake cha awali.
Hao ni makipa; Aishi Manula (Azam FC), Ally Mustafa ‘Barthez’ (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).
Mabeki ni Shomary Kapombe (Azam FC), Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan (Yanga SC), Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka (Simba SC) na Salim Mbonde (Mtibwa Sugar).
Viungo ni Himid Mao, Mudathir Yahya, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo (Azam FC), Jonas Mkude, Said Ndemla (Simba SC) na Salum Telela (Yanga SC). Washambuliaji ni Farid Mussa, John Bocco (Azam FC), Simon Msuva, Malimi Busungu (Yanga SC) na Ibrahim Hajib (Simba SC).
Washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC watajiunga na kambi baada ya mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya USM Alger wikiendi hii mjini Lubumbashi, wakati Mrisho Ngassa wa Free State Stars ya Afrika Kusini atajiunga na kambi mjini Johannersburg.
Elias Maguri wa Stand United ataondoka kesho baada ya kuichezea klabu yake, Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mgambo Shooting Uwanja wa Mkwakwani, Tanga jioni ya leo.
Pamoja na kambi ya mazoezi, Stars inaweza kucheza mchezo mmoja au miwili ya kujipima na wenyeji wao, Bafana Bafana iwapo watakuwa tayari kabla ya kurejea Dar es Salaam Novemba 11 tayari kwa mchezo wa kwanza na Algeria Novemba 14, Uwanja wa Taifa.
Stars itaondoka tena Dar es Salaam kwenda Algiers Novemba 16, tayari kwa mchezo wa marudiano Novemba 17.

Taifa Stars inaondoka leo kwenda Afrika Kusini kwa kambi ya siku 10 |

0 comments:
Post a Comment