// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TAIFA STARS YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA ALGERIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TAIFA STARS YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA ALGERIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, November 14, 2015

    TAIFA STARS YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA ALGERIA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    AMA kweli ng’ombe wa masikini hazai – na mwenye nacho huongezewa. 
    Hayo yamedhihirika leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya Tanzania kuwaruhusu Algeria kusawazisha mabao yote mawili na kupata sare ya 2-2 katika mchezo wa kwanza Raundi ya Pili kufuzu Kombe la Dunia.
    Taifa Stars sasa itahitaji lazima kushinda ugenini Jumanne au kupata sare ya kuanzia 3-3 ili kuingia hatua ya mwisho ya mchujo, ambayo itakuwa ya makundi.
    Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Keita Mahamadou aliyesaidiwa na Diarra Bala na Niare Drissa Kamony wote wa Mali, hadi mapumziko tayari Tanzania walikuwa mbele kwa bao 1-0.
    Mfungaji wa bao la kwanza la Taifa Stars, Elias Maguri (katikati) akipongezwa na wenzake

    Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji Elias Maguri dakika ya 42 kwa kichwa akimalizia krosi beki Mwinyi Hajji Mngwali.
    Stars ingeweza kurudi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ikiwa na mabao zaidi, iwapo Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Farid Mussa wangetumia vyema nafasi nzuri walizopata wakiwa ndani ya boksi la Waalgeria.  
    Kwa ujumla Taifa Stars inayofundishwa na kocha mzalendo, Charles Boniface Mkwasa ilitawala mchezo kipindi cha kwanza na kuwachanganya kabisa wageni.
    Kipindi cha pili, ni Taifa Stars tena iliyorejea uwanjani na moto na kufanikiwa kupata bao la mapema mapema tu dakika ya 54, mfungaji Mbwana Samatta aliyemalizia pasi ya kiungo Mudathir Yahya Abbas.
    Hata hivyo, mabadiliko yaliyofanywa na Kocha Charles Boniface Mkwasa kuwatoa kiungo Mudathir Yahya na mshambuliaji Elias Maguri yaliidhoofisha timu hiyo na kuruhusu wageni kusawazisha.
    Mabao yote ya Algeria yalifungwa na mshambuliaji wake, Slimani Islam dakika ya 71 na 74. Na baada ya kusawazisha Algeria walicharuka zaidi na kukaribia kufunga bao la tatu.
    Mbwana Samatta wa Tanzania akimuacha chini beki wa Algeria, Guediora Aldane
    Kiungo Mudathir Yahya akipambana katikati ya wachezaji wa Algeria
    Thomas Ulimwengu akishirikiana na Farid Mussa kulia kuwatoka mabeki wa Algeria

    Taifa Stars inatarajiwa kuondoka usiku wa manane leo kwa ndege ya Uturuki kwenda Algiers tayari kwa mchezo wa marudiano Jumanne.
    Kikosi cha Taifa Stars kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Himid Mao, Mudathir Yahya/Said Ndemla dk65, Elias Maguri/Mrisho Ngassa dk65 Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Farid Mussa.
    Algeria; M’bolhi Rais, Mandi Issa, Ghoulam Faouzi, Mesloub Wald, Medjani Carl, Zeffanie Mehdi, Guediora Aldane, Tadier Saphir/Belkarou Hichem dk60, Belfodil Isha/Bentaleb Nabil dk46, Slimani Islam/Boudebouda Brahim dk82 na Riyad Mahrez.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA STARS YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA ALGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top