Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KOCHA Muingereza wa Simba SC, Dylan Kerr anaandaa ripoti ya hali halisi ya kikosi chake baada ya hatua ya awali ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, lakini tayari amewaambia viongozi anataka beki mpya wa kati wa kiwango cha kimataifa.
Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo mjini Dar es Salaam kwamba wanatarajiwa kuipata ripoti ya kocha kesho, lakini tayari amewaambia beki ya kati ina tatizo.
“Tunatarajia kuipata ripoti ya kocha kesho, lakini katika mazungumzo ya awali ametuambia kuhusu mahitaji ya beki wa kati na tumekwishaanza kulifanyia kazi,”amesema Aveva.
Aidha, wakati dirisha dogo la usajili linafunguliwa Novemba 15 hadi Desemba 15, mwaka huu, Aveva amesema kwamba wataanza harakati za usajili mara tu watakapopokea ripoti ya kocha.
“Tumejipanga, tena tumejipanga vizuri kuboresha kikosi kwa ajili ya Ligi Kuu na mara tutakapopata tu ripoti ya kocha, tutaanza kuifanyia kazi. Tunatarajia atatuambia tusajili, tunasubiri kujua atahitaji wachezaji wa aina gani,”amesema Aveva.
Kuhusu washambuliaji wawili Warundi, Laudit Mavugo na Kevin Ndayisenga ambao klabu hiyo iliwakosa mwanzoni mwa msimu, Aveva amesema watawarudia iwapo ripoti ya kocha itapendekeza wasajiliwe washambuliaji.
“Tunafahamu kwamba kwa sasa ugumu wa kuwasajili wachezaji hao umepungua. Sasa iwapo ripoti ya kocha itapendekeza wasajiliwe washambuliaji, tutawarudia,”amesema Aveva.
Simba SC ilijaribu kuwasajili kwa wakati tofauti washambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Mavugo na Ndayisenga, lakini maafikiano hayakufikiwa.
Hata hivyo, wachezaji hao wote kwa sasa wamemaliza mikataba na klabu zao Burundi, maana yake kwa kiasi kikubwa gharama za usajili wao zitapungua.
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imesimama kwa muda kupisha maandalizi ya timu ya taifa, Taifa Stars kwa ajili ya michezo ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Algeria.
Taifa Stars ambayo imeweka kambi Afrika Kusini tangu mwanzoni mwa wiki hii, Novemba 14 itaikaribisha Algeria mjini Dar es Salaam kabla ya kurudiana mjini Algiers Novemba 17 na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi kuwania tiketi ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea Desemba 12, mwaka huu, Kagera Sugar wakiikaribisha Ndanda FC, Stand United na Mwadui, Mbeya City na Mtibwa Sugar, Azam FC na Simba SC na Majimaji na Toto Africans, wakati Mgambo JKT watakuwa wenyeji wa Yanga SC na Desemba 13, JKT Ruvu wataikaribisha Prisons na Coastal Union watamenyana na African Sports.

Rais wa Simba SC, Evans Aveva (kushoto) amesema timu inataka beki wa kati wa kimataifa |

0 comments:
Post a Comment