Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MPANGO wa washambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu kwenda Johannesburg, Afrika Kusini kujiunga na kambi ya timu ya taifa umeshindikana na sasa wawili hao wataungana wenzaoe Dar es Salaam.
Taifa Stars iliyoweka kambi Johannesburg, Afrika Kusini kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia katikati ya mwezi huu inatarajiwa kurejea kesho Dar es Salaam– wakati Samatta na Ulimwengu watatu nchini usiku wa leo.
Samatta na Ulimwengu wanakuja kujiunga na kambi ya Stars siku mbili baada ya kuisaidia klabu yao, TP Mazembe ya Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kutwaa ubingwa wa Afrika.
Samatta alifunga bao moja na kuseti moja, TP Mazembe ikitimiza dhamira ya kutwaa ubingwa wa Afrika baada ya kuifunga 2-0 USM Alger ya Algeria Jumapili.
Mchezo huo wa marudiano wa fainali ya Ligi ya Mabingwa uliofanyika Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, wenyeji walipata mabao yote kipindi cha pili.
Na Mazembe inatwaa taji la tano la Ligi ya Mabingwa kwa ushindi wa jumla wa 4-1, baada ya awali kushinda 2-1 mjini Algiers Jumapili iliyopita.
Samatta jana aliwekewa ulinzi mkali na wachezaji wa USM hadi akalazimika kusubiri kufunga bao lake la saba katika michuano ya mwaka huu kwa penalti dakika ya 75, baada ya Rogger Asale kuangushwa.
Samatta naye akamsetia pasi nzuri Assale kufunga bao la pili katika dakika za majeruhi baada ya kutimia dakika 90 za kawaida za mchezo.
Matokeo hayo yanamfanya Samatta pia awe mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa msimu huu, baada ya kufikisha mabao saba, sawa na Bakri Al-Madina wa El-Merreikh ya Sudan.
Hii maana yake huu unakuwa mwaka wa pili mfululizo, Tanzania inatoa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa, baada ya mwaka jana Mrisho Khalfan Ngassa kuongoza pia akiwa na klabu ya Yanga SC, kabla ya kuhamia Free State Stars ya Afrika Kusini msimu huu.
Ngassa alifunga mabao sita sawa na El Hedi Belameiri wa Setif, Haythem Jouini wa Esperance na Ndombe Mubele aliyekuwa AS Vita ya DRC, sasa Al Ahly.
Taifa Stars itaikaribisha Algeria Jumamosi ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya kurudiana mjini Algies Novemba 17 na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi kuwania tiketi ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

Samatta na Ulimwengu wanatarajiwa kuwasili Dar es Salaam usiku wa leo |

0 comments:
Post a Comment