Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
HADI sasa, Mbwana Ally Samatta na Mtanzania mwenzake anayecheza naye TP Mazembe, Thomas Ulimwengu wanajivunia rekodi mpya waliyoweka, kuwa Watanzania wa kwanza kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Na Samatta anajivunia pia rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kufunga bao katika Ligi ya Mabingwa Afrika- baada ya kufunga bao la pili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya USM Alger katika fainali ya kwanza Jumapili iliyopita mjini Algiers.
Awali, Samatta na Ulimwengu walivunja rekodi mbili zilizowekwa na klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam mwaka 1974 na 1993.
1974 Simba SC iliweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza ya Tanzania kucheza Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, walipotolewa na Mehalla El Kubra ya Misri kwa penalti 3-0 baada ya sare ya jumla ya 1-1, kufuatia kila timu kushinda 1-0 nyumbani kwake.
Ni mechi ambayo Simba SC walirejea na malalamiko kwamba kipa wao, Athumani Mambosasa (sasa marehemu) alifanyiwa fujo, wakati wa upigwaji wa penalti ikiwemo kutishiwa bastola.
Mwaka 1993 Simba SC iliweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza ya Tanzania kucheza fainali ya Kikombe cha kwa Afrika kwa ujumla na Kombe la CAF, ambalo sasa limekuwa Kombe la Shirikisho baada ya kuunganishwa na lililokuwa Kombe la Washindi.
Simba SC ilianza vizuri kwa kulazimisha sare ya 0-0 mjini Abidjan, Ivory Coast Novemba 12 dhidi ya Stella kabla ya kufungwa 2-0 mjini Dar es Salaam Novemba 26 mwaka huo.
Samatta na Ulimwengu mwaka 2013 walivunja rekodi ya Simba SC kucheza fainali ya Kombe la CAF walipoichezea Mazembe katika fainali ya Kombe hilo, wakifungwa 2-0 Novemba 23 na CS Sfaxien nchini Tunisia kabla ya kushinda 2-1 Novemba 30 mjini Lubumbashi, Samatta akifunga bao la pili dakika ya 24.
Na msimu huo, Samatta akawa mfungaji bora baada ya kufungana kwa mabao na raia wa Ivory Coast, Vincent Die Foneye aliyekuwa anachezea ENPPI ya Misri, kila mmoja akifunga mabao sita.
Mwaka jana, 2014; Samatta na Ulimwengu wakavunja rekodi ya Simba SC kucheza Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuichezea Mazembe katika hatua hiyo mechi ya kwanza wakifungwa 2-1 Septemba 20 na ES Setif nchini Algeria na marudiano wakashinda 3-2 hivyo Setif kutwaa taji kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya sare ya jumla ya 4-4.
Jumapili iliyopita Samatta na Ulimwengu wakaandika rekodi mpya ya kuwa Watanzania wa kwanza kucheza Fainali ya Ligi ya Mabingwa, huku Mbwana pia akiweka rekodi binafsi ya kufunga bao katika mechi hiyo Algiers.
Leo, Mazembe wakiikaribisha USM Alger na mtaji wao wa ushindi wa 2-1 ugenini, Samatta na Ulimwengu wanawania kuwa Watanzania wa kwanza kutwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika.
Lakini pia Mbwana anawania kuwa Mtanzania wa pili kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo, baada ya Mrisho Ngassa aliyekuwa Yanga SC mwaka jana, kabla ya kuhamia Free State Stars ya mwaka huu.
Ngassa alikuwa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu kwa kufunga mabao sita akifungana na El Hedi Belameiri wa Setif, Haythem Jouini wa Esperance na Ndombe Mubele aliyekuwa AS Vita ya DRC, sasa Al Ahly.
Hadi sasa Samatta ana mabao sita, akizidiwa moja na Sudan Bakri Al-Madina wa El-Merreikh ya Sudan. Samatta analingana na Mmorocco Mouhcine Iajour wa Moghreb Tetouan ya kwao, wakati Muivory Coast wa Mazembe pia, Roger Assale ana mabao matano.
Je, Mbwana Ally Samatta atavunja rekodi ya Ngassa leo? Bila shaka hizo ndizo dua za Watanzania kwa vijana wao hao leo.

Mbwana Samatta atakuwa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika leo? |

Mrisho Ngassa ni mfungaji bora wa msimu uliopita Ligi ya Mabingwa Afrika |
Lakini pia Mbwana anawania kuwa Mtanzania wa pili kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo, baada ya Mrisho Ngassa aliyekuwa Yanga SC mwaka jana, kabla ya kuhamia Free State Stars ya mwaka huu.
Ngassa alikuwa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu kwa kufunga mabao sita akifungana na El Hedi Belameiri wa Setif, Haythem Jouini wa Esperance na Ndombe Mubele aliyekuwa AS Vita ya DRC, sasa Al Ahly.
Hadi sasa Samatta ana mabao sita, akizidiwa moja na Sudan Bakri Al-Madina wa El-Merreikh ya Sudan. Samatta analingana na Mmorocco Mouhcine Iajour wa Moghreb Tetouan ya kwao, wakati Muivory Coast wa Mazembe pia, Roger Assale ana mabao matano.
Je, Mbwana Ally Samatta atavunja rekodi ya Ngassa leo? Bila shaka hizo ndizo dua za Watanzania kwa vijana wao hao leo.
0 comments:
Post a Comment