REKODI YA TANZANIA NA ALGERIA
Januari 8, 1973;
Algeria 4-2 Tanzania (AAG Lagos)
Januari 21, 1995;
Tanzania 2-1 Algeria (AFCON Dar)
Julai 28, 1995;
Algeria 2-1 Tanzania (AFCON Algiers)
Oktoba 4, 1997;
Tanzania 0-1 Algeria (Kombe la Sumaye)
Agosti 18, 2002;
Algeria 0-0 Tanzania (Kirafiki)
Septemba 3, 2010;
Algeria 0-0 Tanzania (AFCON Algiers)
Septemba 3, 2011;
Tanzania 1-1 Algeria (AFCON Dar)
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
WAKATI kesho Tanzania watakuwa wenyeji wa Algeria katika mchezo wa kwanza Raundi ya Pili kufuzu Kombe la Dunia, hofu imetawala kwa wenyeji juu ya wapinzani wao ambao kwa sasa wanashika nafasi ya pili kwa ubora wa soka barani.
Baadhi wanaamini Taifa Stars itashuka uwanjani kesho kutekeleza wajibu tu – lakini tayari wamekwishafungwa kutokana na imani kwamba Mbweha wa Jangwani ni bora zaidi.
Pamoja na hofu hiyo, lakini rekodi ya mechi zilizotangulia baina ya timu hizo inaonyesha michezo yote miwili, wa Dar es Salaam kesho na Algiers Jumanne ni migumu na haitabiriki.
Kabla ya mchezo wa kesho, tayari Algeria na Tanzania zimekwishakutana mara saba na mechi zote timu hizo zilitoana jasho, ingawa Taifa Stars imefungwa zaidi.
Tanzania imeifunga Algeria mara moja tu Januari 21 mwaka 1995 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zilizofanyika mwaka 1996 Afrika Kusini.
Huo ulikuwa mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) Dar es Salaam na marudiano, Algeria ikashinda 2-1 Julai 28, mwaka 1995 mjini Algiers, hiyo ilikuwa hatua ya makundi ya mtoano.
Kabla ya hapo, timu hizo zilikutana mara ya kwanza kabisa katika Michezo ya Afrika (All Africans Games) mjini Lagos, Nigeria Januari 8, mwaka 1973 na Algeria ikashinda 4-2.
Timu hizo zikaja kukutana tena katika mchezo wa michuano ya ufunguzi wa Uwanja wa Uhuru baada ya ukarabati, iliyopewa jina Kombe la Sumaye na Algeria ikashinda 1-0 Dar es Salaam Oktoba 4, mwaka 1997.
Timu hizo zikaja kukutana tena katika mechi ya kirafiki ya kimataifa Agosti 18 mwaka 2002 na kutoa sare ya bila kufungana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Zikakutana tena Septemba 3, mwaka 2010 kuwania tiketi ya Mataifa ya Afrika na kutoa sare ya 0-0 Algiers wakati marudiano Septemba 3 mwaka 2011, timu hizo zikatoa tena sare ya 1-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na huo ndiyo ulikuwa mchezo wa mwisho timu hizo kukutana.
Zinakutana kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili kufuzu Kombe la Dunia kabla ya kurudiana Jumanne mjini Algiers.
Je, nani ataibuka mshindi wa jumla na kufuzu hatua ya mwisho ya mchujo wa mbio za Urusi 2018?
Januari 8, 1973;
Algeria 4-2 Tanzania (AAG Lagos)
Januari 21, 1995;
Tanzania 2-1 Algeria (AFCON Dar)
Julai 28, 1995;
Algeria 2-1 Tanzania (AFCON Algiers)
Oktoba 4, 1997;
Tanzania 0-1 Algeria (Kombe la Sumaye)
Agosti 18, 2002;
Algeria 0-0 Tanzania (Kirafiki)
Septemba 3, 2010;
Algeria 0-0 Tanzania (AFCON Algiers)
Septemba 3, 2011;
Tanzania 1-1 Algeria (AFCON Dar)
Mshambuliaji wa Tanzania, Danny Mrwanda akimuacha chini beki wa Algeria katika mchezo wa kufuzu AFCON Septemba 3, mwaka 2011 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka 1-1 |
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
WAKATI kesho Tanzania watakuwa wenyeji wa Algeria katika mchezo wa kwanza Raundi ya Pili kufuzu Kombe la Dunia, hofu imetawala kwa wenyeji juu ya wapinzani wao ambao kwa sasa wanashika nafasi ya pili kwa ubora wa soka barani.
Baadhi wanaamini Taifa Stars itashuka uwanjani kesho kutekeleza wajibu tu – lakini tayari wamekwishafungwa kutokana na imani kwamba Mbweha wa Jangwani ni bora zaidi.
Pamoja na hofu hiyo, lakini rekodi ya mechi zilizotangulia baina ya timu hizo inaonyesha michezo yote miwili, wa Dar es Salaam kesho na Algiers Jumanne ni migumu na haitabiriki.
Kabla ya mchezo wa kesho, tayari Algeria na Tanzania zimekwishakutana mara saba na mechi zote timu hizo zilitoana jasho, ingawa Taifa Stars imefungwa zaidi.
Tanzania imeifunga Algeria mara moja tu Januari 21 mwaka 1995 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zilizofanyika mwaka 1996 Afrika Kusini.
Huo ulikuwa mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) Dar es Salaam na marudiano, Algeria ikashinda 2-1 Julai 28, mwaka 1995 mjini Algiers, hiyo ilikuwa hatua ya makundi ya mtoano.
Kabla ya hapo, timu hizo zilikutana mara ya kwanza kabisa katika Michezo ya Afrika (All Africans Games) mjini Lagos, Nigeria Januari 8, mwaka 1973 na Algeria ikashinda 4-2.
Timu hizo zikaja kukutana tena katika mchezo wa michuano ya ufunguzi wa Uwanja wa Uhuru baada ya ukarabati, iliyopewa jina Kombe la Sumaye na Algeria ikashinda 1-0 Dar es Salaam Oktoba 4, mwaka 1997.
Timu hizo zikaja kukutana tena katika mechi ya kirafiki ya kimataifa Agosti 18 mwaka 2002 na kutoa sare ya bila kufungana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Zikakutana tena Septemba 3, mwaka 2010 kuwania tiketi ya Mataifa ya Afrika na kutoa sare ya 0-0 Algiers wakati marudiano Septemba 3 mwaka 2011, timu hizo zikatoa tena sare ya 1-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na huo ndiyo ulikuwa mchezo wa mwisho timu hizo kukutana.
Zinakutana kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili kufuzu Kombe la Dunia kabla ya kurudiana Jumanne mjini Algiers.
Je, nani ataibuka mshindi wa jumla na kufuzu hatua ya mwisho ya mchujo wa mbio za Urusi 2018?
0 comments:
Post a Comment