BAO pekee la Farouk Miya dakika ya 39 limeipa Uganda ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji, Togo katika mchezo wa kwanza Raundi ya Pili kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi.
Ushindi wa ugenini unaipa Korongo nafasi nzuri ya kuingia hatua ya mwisho ya mchujo baada ya mchezo wa marudiano Jumapili mjini Kampala, Uganda.
Wachezaji wote wa Simba SC, beki Juuko Murushid na mshambuliaji wa Simba SC, Hamisi Kizza wamecheza jioni ya leo Uwanja wa Kegue mjini Lome. Juuko alicheza dakika zote 90, wakati Kizza alianza mechi hiyo kabla ya kumpisha Brian Umony dakika ya 56.
Beki wa Yanga SC, Vincent Bossou wa Togo alikuwa benchi kwa muda wote wa mchezo huo timu yake ikifungwa nyumbani.
Timu zote zilikutanisha makocha wa zamani wa klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam, Togo ya Mbelgiji Tom Saintfiet na Uganda ya Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’.
Burundi imefungwa mabao 3-2 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya KOngo (DRC) katika mchezo wa kwanza Raundi ya Pili kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Mabao ya Burundi yamefungwa na Cedric Amissi dakika ya 38 na 83, wakati ya DRC yamefungwa na Yannick Bolasie Yala dakika ya tano, Firmin Ndombe Mubele dakika za 86 na 88.
Bao pekee la Naby Deco Keita dakika ya 27 limeipa Guinea ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Namibia, wakati Benin imeshinda 2-1 nyumbani dhidi ya Burkina Faso. Mabao ya Benin yamefungwa na Stephane Sessegnon kwa penalti dakika ya 45 na ushei na Bello Issiaka Babatounde dakika ya 84, wakati la Burkinabe limefungwa na Prejuce Niguimbe Nakoulma dakika ya 51.
Mechi za jana, timu za kusini mwa Afrika, Msumbiji na Zambia jana zimepata ushindi mwembamba wa 1-0 kila timu katika mechi za kwanza za Raundi ya Pili kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi.
Bao la dakika ya 55 la Helder Pelembe limeipa Mambas (Nyoka) ushindi wa 1-0 dhidi ya Gabon Uwanja wa Zimpeto mjini Maputo.
Gabon ilimkosa mshambuliaji wake nyota, Pierre-Emerick Aubameyang wa Borussia Dortmund ya Ujerumani anayesumbuliwa na maumivu ya misuli – ambaye ameifungia nchi yake mabao 22 katika mechi 20.
Kipa wa Sudan, Akram El Hadi Salim na beki Ramadan Agab watabeba lawama kwa pamoja kwa kuiruhusu Zambia kupata bao pekee kwa makosa yao.
Kila mmoja alimsubiri mwenzake aokoea mpira kwenye eneo la penalti na Kalengo akauwahi kuifungia timu yake Uwanja wa Karima.
Ushindi huo unaiweka Zambia katika nafasi nzuri ya kufuzu katika hatua ya mwisho wa mchujo baada ya mcheo wa marudiano mjini Ndola Jumapili.
Mechi zaidi za kufuzu Kombe la Dunia zinatarajiwa kuendelea kesho na keshokutwa. Tanzania itawakribisha Algeria Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hamisi Kizza amecheza leo Uganda ikishinda 1-0 ugenini dhidi ya Togo |

0 comments:
Post a Comment