WACHEZAJI wawili wa Simba SC, beki Juuko Murushid na mshambuliaji Hamisi Kizza ‘Diego’ wamejumuishwa kwenye kikosi cha mwisho cha Uganda, ‘The Cranes’ kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Togo.
Korongo wa Uganda wataanzia ugenini Uwanja wa Kegue mjini Lome Alhamisi kabla ya kurudiana Jumapili Uwanja wa Taifa wa Mandela, eneo la Namboole mjini Kampala, Uganda na mshindi wa jumla atafuzu kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi.
Kocha wa Uganda, Mserbia Milutin ‘Micho’ Sredojevic ametaja kikosi kitakachosafiri kwenda Togo baada ya mazoezi ya mwisho leo Uwanja wa Chuo cha Vienna eneo la Namugongo, Kampala.
Kikosi hicho kinaundwa na makipa; Onyango Denis, Odongkara Robert, mabeki; Iguma Denis, Isaac Isinde, Walusimbi Godfrey, Juuko Murushidi na Ivan Bukenya.
Viungo ni Khalid Aucho, Kizito Luwagga, Miya Farouk, Brian Umony, Massa Geoffrey, Kizito Geoffrey na Oloya Moses – wakati washambuliaji ni Kizza Hamisi,Tonny Mawejje, Okhuti Caesar na Ochaya Joseph.
Msafara wa Uganda utaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Soka nchini humo (FUFA), Hamid Juma na utaondoka Saa 4:00 asubuhi kesho kwa ndege.

Mshambuliaji tegemeo wa Simba SC, Hamisi Kizza atakwenda na Uganda nchini Togo |
Kocha wa Uganda, Mserbia Milutin ‘Micho’ Sredojevic ametaja kikosi kitakachosafiri kwenda Togo baada ya mazoezi ya mwisho leo Uwanja wa Chuo cha Vienna eneo la Namugongo, Kampala.
Kikosi hicho kinaundwa na makipa; Onyango Denis, Odongkara Robert, mabeki; Iguma Denis, Isaac Isinde, Walusimbi Godfrey, Juuko Murushidi na Ivan Bukenya.
Viungo ni Khalid Aucho, Kizito Luwagga, Miya Farouk, Brian Umony, Massa Geoffrey, Kizito Geoffrey na Oloya Moses – wakati washambuliaji ni Kizza Hamisi,Tonny Mawejje, Okhuti Caesar na Ochaya Joseph.
Msafara wa Uganda utaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Soka nchini humo (FUFA), Hamid Juma na utaondoka Saa 4:00 asubuhi kesho kwa ndege.
0 comments:
Post a Comment