KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa (pichani kulia) amecheza dakika zote 90 klabu yake, Free State Stars ikilazimishwa sare ya 0-0 na SuperSport United jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini, uliofanyika Uwanja wa Goble Park mjini Bethlehem.
Na Ngassa aliyecheza vizuri eneo la kiungo mchezeshaji, alifumua shuti kali dakika ya 28 langoni mwa wapinzani, lakini likaenda nje sentimita chache.
Free State sasa inashika nafasi ya 10 katika msimamo wa ABSA wa timu 16, baada ya kuvuna pointi 11 katika mechi nane, wakati SuperSport yenye pointi tisa za mechi tisa ni ya 11.
Kikosi cha Stars kilikuwa: Diakite, Masehe, Mashego, Shabalala, Sankara/Mohomi dk67, Tlhone, Ngassa, Sekola/Somaeb dk75, Fileccia/Thethani dk76, Kerspuy na Venter.
United: Williams, Khumalo, Daniels, Farmer, Kekana, Mkhabela/Grobler dk62, Furman, Lakay/Rambuwane dk58, Wome, Phala na Brockie.

0 comments:
Post a Comment