Na Harakandi Patrick, BUJUMBURA
MSHAMBULIAJI Mrundi, Kevin Ndayisenga amesema kwamba yuko tayari kurejea Simba SC wakati wowote iwapo itafikia makubaliano na Meneja wake, Dennis Kadito.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE mjini hapa jana, Ndayisenga amesema kwamba awali alishindwa kusaini Simba SC baada ya klabu hiyo kushindwa kufikia makubaliano na Meneja wake, Kadito.
“Kama watazungumza na Kadito vizuri, wakakubaliana mimi nitakwenda kucheza kule, ni klabu kubwa na ina mashabiki wengi, ninaipenda,”alisema.
Simba SC ilikaribia kumsajili Ndayisenga Agosti mwaka huu, lakini ikashindwa kufikia makubaliano na Meneja wake, Kadito baada ya mchezaji huyo kufaulu majaribio ya wiki moja.
Kwa sasa Ndayisenga hachezi Ligi nchini Burundi kutokana na kumaliza Mkataba na klabu yake, Bujumbura City.
Na Mpango wa kumsajili Ndayisenga ulikuja Simba SC baada ya kumkosa mshambuliaji mwingine wa Burundi, Laudit Mavugo kwa sababu ya dau pia.
Baada ya kuwakosa wote, Simba SC ilimsajili Msenegali, Abdoulaye Pape N’daw aliyekwenda kuungana na Vincent Angban (Ivory Coast), Emery Nimubona (Burundi), Juuko Murushid (Uganda), Justice Majabvi (Zimbabwe), Simon Sserunkuma (Uganda) na Hamisi Kizza (Uganda) kukamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Hata hivyo, inaonekana kabisa Simba SC haijaridhishwa na N’daw na wakati huo huo winga Mganda, Sserunkuma hajawa na msaada kwenye timu hiyo- maana yake inaweza kuwaacha wawili hao wote Desemba na kusajili wachezaji wengine.

Kelvin Ndayisenga alifanya vizuri katika majaribio yake Simba SC |

0 comments:
Post a Comment