Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
“Mungu ibariki Tanzania, Dumisha uhuru na Umoja, Wake kwa Waume na Watoto, Mungu Ibariki Tanzania na watu wake,”.
“Ibariki Tanzania, Ibariki Tanzania, Tubariki watoto wa Tanzania,” Amin.
Huu ni wimbo wa taifa la Tanzania ambao utapigwa leo na kuimbwa kwa hisia na maelfu ya wananchi Uwanja wa Taifa wa mjini Dar es Salaam kabla ya mchezo wa soka dhidi ya Algeria.
Tanzania ‘Taifa Stars’ wanacheza na Algeria kuanzia Saa 10:00 jioni ya leo Uwanja wa Taifa katika mchezo wa kwanza Raundi ya Pili kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi, kabla ya kurudiana Jumanne mjini Algiers na mshindi wa jumla atasonga hatua ya mwisho ya mchujo, ambayo itakuwa ya makundi.
Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais Dk Samia Hassan Suluhu wanatarajiwa kuwaongoza Watanzania wengine kuisapoti Taifa Stars leo.
Ilikuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk, John Pombe Joseph Magufuli naye awepo kama si kupata msiba wa mjukuu wake, Maryfaustna Mlyambina, aliyefariki Jumatano (Novemba 11, 2015), Kimara mjini Dar es Salaam na kusafirishwa mkoani Mwanza kwa mazishi jana.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema vijana wake wapo tayari kwa mchezo huo baada ya maandalizi ya takriban siku 10, ikiwemo kambi ya wiki moja Afrika Kusini.
Wachezaji wote wameonyesha dhamira na nia ya kucheza kwa bidii leo ili kufuzu huo mgumu.
Washambuliaji tegemeo Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu waliochelewa kujiunga na wenzao kutokana na kusubiri fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika walifanya mazoezi na wenzao juzi na jana.
Wawili hao waliwasili Dar es Salaam Jumatano baada ya kuisaidia Mazembe kutwaa ubingwa wa Afrika wakiifunga USM Alger ya Algeria jumla ya mabao 4-1, Samatta akifunga mawili, moja ugenini na moja nyumbani na pia kuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo.
Mchezo wa leo utakuwa wa nane kihistoria kuzikutanisha timu hizo, Tanzania ikishinda mara moja, kutoa sare tatu na kufungwa tatu.
Taifa Stars iliifunga Algeria Januari 21 mwaka 1995 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zilizofanyika mwaka 1996 Afrika Kusini wakati marudiano Algeria ilishinda 2-1 Julai 28, mwaka 1995 mjini Algiers, hiyo ilikuwa hatua ya makundi ya mtoano.
Kabla ya hapo, timu hizo zilikutana mara ya kwanza kabisa katika Michezo ya Afrika (All Africans Games) mjini Lagos, Nigeria Januari 8, mwaka 1973 na Algeria ikashinda 4-2.
Timu hizo zikaja kukutana tena katika mchezo wa michuano ya ufunguzi wa Uwanja wa Uhuru baada ya ukarabati, iliyopewa jina Kombe la Sumaye na Algeria ikashinda 1-0 Dar es Salaam Oktoba 4, mwaka 1997.
Timu hizo zikaja kukutana tena katika mechi ya kirafiki ya kimataifa Agosti 18 mwaka 2002 na kutoa sare ya bila kufungana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Zikakutana tena Septemba 3, mwaka 2010 kuwania tiketi ya Mataifa ya Afrika na kutoa sare ya 0-0 Algiers wakati marudiano Septemba 3 mwaka 2011, timu hizo zikatoa tena sare ya 1-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na huo ndiyo ulikuwa mchezo wa mwisho timu hizo kukutana.
Taifa Stars ikeweka kambi katika hoteli ya Serena tangu imewasili kutoka Johannesburg, Afrika Kusini wakati Mweha wa Jangwani wamefikia hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro Kempenski).
Mechi mbili zilizopita, Tanzania iliifunga Malawi 2-0 Dar es Salaam kabla ya kufungwa na timu hiyo 1-0 Blantyre, wakati Algeria ilifungwa na Guinea 2-1 kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya Senegal, zote za kirafiki.
Kikosi cha Taifa Stars kinatarajiwa kuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Himid Mao, Mudathir Yahya, Salum Abubakar, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Mrisho Ngassa.
Algeria; Azzedine Doukha, Mohamed Khouti Ziti, Hichem Belkaroui, Carl Medjani, Yacine Brahimi, Ryad Boudebouz, Sofiane Feghouli, Walid Mesloub, Saphir Sliti Taider, Riyad Mahrez na Baghdad Bounedjah.
Mungu ibariki Tanzania iifunge Algeria. Amin.

Mungu ibariki Taifa Stars leo iifunge Algeria, mambo mengine yatafuata |

Mbwana Samatta (kulia) leo anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji Taifa Stars |
Taifa Stars iliifunga Algeria Januari 21 mwaka 1995 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zilizofanyika mwaka 1996 Afrika Kusini wakati marudiano Algeria ilishinda 2-1 Julai 28, mwaka 1995 mjini Algiers, hiyo ilikuwa hatua ya makundi ya mtoano.
Kabla ya hapo, timu hizo zilikutana mara ya kwanza kabisa katika Michezo ya Afrika (All Africans Games) mjini Lagos, Nigeria Januari 8, mwaka 1973 na Algeria ikashinda 4-2.
Timu hizo zikaja kukutana tena katika mchezo wa michuano ya ufunguzi wa Uwanja wa Uhuru baada ya ukarabati, iliyopewa jina Kombe la Sumaye na Algeria ikashinda 1-0 Dar es Salaam Oktoba 4, mwaka 1997.
Timu hizo zikaja kukutana tena katika mechi ya kirafiki ya kimataifa Agosti 18 mwaka 2002 na kutoa sare ya bila kufungana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Zikakutana tena Septemba 3, mwaka 2010 kuwania tiketi ya Mataifa ya Afrika na kutoa sare ya 0-0 Algiers wakati marudiano Septemba 3 mwaka 2011, timu hizo zikatoa tena sare ya 1-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na huo ndiyo ulikuwa mchezo wa mwisho timu hizo kukutana.
Taifa Stars ikeweka kambi katika hoteli ya Serena tangu imewasili kutoka Johannesburg, Afrika Kusini wakati Mweha wa Jangwani wamefikia hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro Kempenski).
Mrisho Ngassa anatarajiwa kuanza leo dhidi ya Algeria |
Mechi mbili zilizopita, Tanzania iliifunga Malawi 2-0 Dar es Salaam kabla ya kufungwa na timu hiyo 1-0 Blantyre, wakati Algeria ilifungwa na Guinea 2-1 kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya Senegal, zote za kirafiki.
Kikosi cha Taifa Stars kinatarajiwa kuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Himid Mao, Mudathir Yahya, Salum Abubakar, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Mrisho Ngassa.
Algeria; Azzedine Doukha, Mohamed Khouti Ziti, Hichem Belkaroui, Carl Medjani, Yacine Brahimi, Ryad Boudebouz, Sofiane Feghouli, Walid Mesloub, Saphir Sliti Taider, Riyad Mahrez na Baghdad Bounedjah.
Mungu ibariki Tanzania iifunge Algeria. Amin.
Thomas Ulimwengu mwenye nguvu na kasi anatarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa Stars leo |
0 comments:
Post a Comment