// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ‘MADOGO’ WA SAUZI WAITUNGUA TAIFA STARS 2-0 JO’BURG - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ‘MADOGO’ WA SAUZI WAITUNGUA TAIFA STARS 2-0 JO’BURG - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, November 10, 2015

    ‘MADOGO’ WA SAUZI WAITUNGUA TAIFA STARS 2-0 JO’BURG

    TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefungwa mabao 2-0 na U23 ya Afrika Kusini katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jioni ya leo Uwanja wa Eldorado mjini Johanesburg, Afrika Kusini.
    Huo ulikuwa mchezo pekee wa kujipima nguvu katika kambi ya wiki moja na ushei ya Taifa Stars mjini Johannesburg kujiandaa na mchezo dhidi ya Algeria Jumamosi wiki hii.
    Na kocha Mkuu wa timu hiyo, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba kufungwa huko kulitokana na wachezaji wake kucheza kwa tahadhari kuhofia kuumia kabla ya mechi muhimu dhidi ya Algeria.

    Katika mchezo wa leo, Mkwasa alimchezesha kipa 
    Aishi Manula, badala ya Ally Mustafa ‘Barthez’ ambaye amekuwa akimtumia mechi zilizopita, wakati safu ya ulinzi ilikuwa ile ile ya siku zote.
    Kwa ujumla kikosi cha Stars kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Jonas Mkude/Himid Mao, Simon Msuva, Salum Abubabar ‘Sure Boy’/Frank Domayo, John Bocco/Elius Maguri, Mrisho Ngassa/Malimi Busungu na Farid Mussa/Salum Telela.
    Baada ya mchezo huo, Taifa Stars inatarajiwa kurejea Dar es Salaam kesho na itafikia hoteli ya Serena – na itaendelea na mazoezi ya mwisho Uwanja wa Taifa.
    Tanzania, ‘Taifa Stars’ itamenyana na Algeria, ‘Mbweha wa Jangwani’ Jumamosi kabla ya kurudiana Novemba 17 mjini Algiers na mshindi wa jumla ataingia kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia 2018 Urusi.
    Algeria, timu namba moja kwa ubora wa soka Afrika kwa sasa, inatarajiwa kuwasili nchini Alhamisi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ‘MADOGO’ WA SAUZI WAITUNGUA TAIFA STARS 2-0 JO’BURG Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top