MSHAMBULIAJI chipukizi wa England, Jamie Vardy amekuwa mchezaji wa kwanza wa Leicester City kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu ya England kwa miaka 15.
Vardy ametwaa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao matano katika mechi nne za Leicester City za Ligi Kuu ya England mwezi uliopita.
Kipa wa zamani wa England, Tim Flowers alikuwa mchezaji wa mwisho wa Leicester City kutwaa tuzo hiyo Septemba mwaka 2000 baada ya kufungwa mabao mawili tu na kuiweka kileleni timu hiyo kwa kukusanya pointi 16 katika mechi nane, wakati chini ya kocha Peter Taylor.
Kocha Mfaransa wa Arsenal, Arsene Wenger ametwaa tuzo ya Kocha Bora wa mwezi baada ya kuiongoza timu hiyo kukabana koo na Manchester City kileleni katika Ligi Kuu ya England.
Mshambuliaji wa Leicester City, Jamie Vardy akiwa na tuzo yake ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya England mwezi Oktoba PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment