Zlatan Ibrahimovic akiwa na tuzo yake Mwanasoka Bora wa Sweden ambayo ameitwaa mara ya tisa mfululizo tangu alipoichukua kutoka kwa Fredrik Ljungberg mwaka 2006 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Sweden kwa mara ya 10 katika historia yake na mara ya tisa mfululizo.
Na baada ya ushindi wa tuzo hiyo, mchezaji huyo mwenye nguvu, amewataka wachezaji wenzake kujitolea kila kitu katika mchezo wa mchujo wa kufuzu wa Euro 2016 dhidi ya Denmark.
Mpachika mabao huyo wa Paris St Germain alikuwa ana mwaka mzuri uliopita, akishinda taji la Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1 likiwa taji lake la 12 la ligi kushinda huku akifunga mabao 30 katika mechi 35.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Inter Milan na Barcelona mwenye umri wa miaka 34, wiki hii atakuwa na mtihani mgumu kwa ajili ya taifa lake, atakapoipigania Sweden tiketi ya Fainali za Mataifa ya Ulaya mwakani watakapomenyama na Denmark katika mchezo wa mwisho wa kufuzu.
0 comments:
Post a Comment