Tenga kulia akimkaribisha Dk. Jaffer |
Mutasim amepata kura sita kati ya 10 dhidi ya wapinzani wake, Mganda Lawrence Mulindwa aliyeoata kura tatu na Vincent Nzamwita wa Rwanda aliyeambulia kura moja, wakati Junedin Basha wa Ethiopia alijitoa kwenye uchaguzi huo dakika za mwishoni.
Katika hotuba yake ya kumkaribisha Rais mpya, Tenga alisema Jaffer ni mtu anayefaa kuongoza CECAFA.
"Nina furaha kukabidhi madaraka kwa mtu ambaye ni mweledi na anapenda soka. Tunataka kuona CECAFA inakuwa katika michache ijayo na kunufaika na programu mpya za maendeleo za FIFA,"amesema Tenga.
"Nina furaha nimefanya mazuri katika miaka yangu minane iliyopita kama Rais, lakini nitakuwa tayari wakati wowote kwa ushauri nikihitajika,” amesema Tenga.
Kwa upande wake, Rais mpya wa CECAFA, Jaffer amesema kwamba anatarajia kuinua kiwango cha soka ya ukanda huu kimataifa.
"Uchaguzi huu hauna mshindi wala washindwa, naamini sisi ni familia moja na ninataka haraka kuingia kazini kubadiliosha mwonekano wa soka ya nchi wanachama za CECAFA na kuhakikisha tunayapatia udhamini mashindano yote, kuanzia ya vijana chini ya umri wa miaka 17 hadi ya wakubwa,"amesema.
Uchaguzi wa CECAFA umefanyika Addis Ababa, Erhiopia jana ambako leo michuano ya Kombe la Challenge inaanza.
0 comments:
Post a Comment