Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC ipo katika mazungumzo na klabu tofauti za Asia na Ulaya ambazo zinataka kununua wachezaji wake watatu, beki Mtogo Vincent Bossou, kiungo Mbrazil Andrey Coutinho na mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma.
BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE inafahamu Yanga SC ipo kwenye mazungumzo na klabu mbili za Malaysia ambazo zinawataka Bossou na Coutinho.
Aidha, klabu moja nchini Denmark imeonyesha nia ya dhati ya kumnunua mshambuliaji Ngoma na mazungumzo yanaendelea na klabu yake.
Baada ya mazungumzo ya awali, Yanga SC wameziagiza klabu zote hizo ziandike barua rasmi za ofa za kuwataka wachezaji hao.
Coutinho yupo katika msimu wake wa pili Yanga SC hadi sasa akiwa ameichezea timu hiyo mechi 36 na kufunga mabao saba, wakati Ngoma na Bossou wote wapo katika msimu wao wa kwanza Jangwani.
Hadi sasa, Ngoma amekwishaifungia Yanga SC mabao 12 katika mashindano yote katika 18 alizoichezea timu hiyo, wakati Bossou ameichezea mechi tatu tu timu hiyo.
Wakati huo huo, kuna wachezaji watatu vijana wadogo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wametua Yanga kwa majaribio.
Hata hivyo, wachezaji hao ambao wamekwishaanza kufanya mazoezi na timu ya vijana ya Yanga SC, labda wanaweza wakapata nafasi ya majaribio kikosi cha kwanza wiki ijayo timu hiyo itakaporejea mazoezini.

Mshambuliaji Donald Ngoma anatakiwa na klabu ya Denmark |

0 comments:
Post a Comment