![]() |
Mshambuliaji wa Yanga SC, Amissi Tambwe amwfunga bao jana Challenge |
Mshambuliaji wa Yanga SC, Amissi Tambwe alianza kuifungia Burundi dakika ya 11 kabla ya mpachika mabao wa Gor Mahia, Michael Olunga kuisawazishia Kenya dakika ya 41.
Mchezo wa Kundi A, wenyeji Ethiopia wameshinda 2-0 dhidi ya Somalia mabao ya Mohammed Nasser na Behailu Girma.
Mechi za Kundi C, Malawi imeichapa mabao 3-0 Djibouti, mabao ya Gerlad Phiri Jnr, John Banda na Chiukepo Msowoya wakati Sudan Kusini imetoka sare ya 0-0 na Sudan.
Leo ni mapumziko na kesho mechi za makundi zinatarajiwa kuhitimishwa kwa mechi kati ya Rwanda Vs Somalia, Zanzibar Vs Kenya, Sudan Kusini Vs Malawi, Djibouti Vs Sudan, Uganda Vs Burundi na Tanzania Vs Ethiopia.
0 comments:
Post a Comment