MATOKEO NA RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
Oktoba 31, 2015
Simba SC 6-1 Majimaji FC
Kagera Sugar 0-2 Yanga SC
Mtibwa Sugar 4-1 Mwadui FC
Coastal Union 1-1 Mbeya City
Novemba 1, 2015
Prisons Vs Ndanda FC
African Sports Vs JKT Ruvu
Azam FC Vs Toto Africans
Novemba 2, 2015
|
YANGA SC imefanikiwa kurejea juu ya msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar ya Bukoba Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora jioni ya leo.
Ushindi huo, unaifanya timu hiyo ya kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm ifikishe pointi 23, baada ya kucheza mechi tisa, ikiizidi kwa pointi moja Azam FC, ambayo itacheza mechi ya tisa kesho dhidi ya Toto Africans.
Yanga SC ilipata bao lake la kwanza dakika ya 23 kupitia kwa Mzimbabwe, Donald Dombo Ngoma aliyemalizia kwa kichwa krosi ya beki wa Juma Abdul, ambaye naye alipenyezewa mpira pembeni na Deus Kaseke.
Hilo linakuwa bao la nane kwa Ngoma msimu huu na sasa analingana na Elias Maguri wa Stand United na Hamisi Kizza wa Simba SC wanaoongoza kwa mabao Ligi Kuu.
Bao la pili lilifungwa na kiungo Deus Kaseke dakika ya 63 aliyemalizia mpira uliookolewa na kipa Agaton Anthony baada ya Amissi Tambwe kuunganisha krosi ya Simon Msuva.
Kagera Sugar waliamua kuacha kucheza kwa kujihami baada ya kufungwa bao hilo na kwenda kushambulia langoni mwa Yanga SC na wakakaribia kufunga mara mbili.
Ngoma, Tambwe na Msuva nao wote walikaribia kuifungia Yanga SC.
Kikosi cha Kagera Sugar kilikuwa; Kagera Sugar; Agatony Anthony, Salum Kanoni, Abdil Mtiro, Ibrahim Job, Joseph James, George Kavilla, Juma Mpola, Iddi Kurachi, Alhaji Zege/Kenneth Masumbuko dk46, Paul Ngalyoma na Mbaraka Yusuph.
Yanga SC; Deo Munish ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Kevin Yondan, Vicent Bossou, Mbuyu Twitte, Malimi Busungu/Simon Msuva dk54, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Donald Ngoma/mateo Anthony dk88 na Deus Kaseke/Godfrey Mwashiuya dk85.
0 comments:
Post a Comment