// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC WAWAOMBA RADHI MASHABIKI, WASEMA HAWATARUDIA MAKOSA TENA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC WAWAOMBA RADHI MASHABIKI, WASEMA HAWATARUDIA MAKOSA TENA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Friday, October 30, 2015

        YANGA SC WAWAOMBA RADHI MASHABIKI, WASEMA HAWATARUDIA MAKOSA TENA

        MECHI ZIJAZO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
        Oktoba 31, 2015
        Simba SC Vs Majimaji FC
        Kagera Sugar Vs Yanga SC
        Mtibwa Sugar Vs Mwadui FC
        Prisons Vs Ndanda FC
        Coastal Union Vs Mbeya City
        Novemba 1, 2015
        African Sports Vs JKT Ruvu
        Azam FC Vs Toto Africans
        Novemba 2, 2015
        Mgambo Shooting Vs Stand United
        Wachezaji wa Yanga SC wamewaomba radhi mashabiki wao 

        Na Prince Akbar, TABORA
        NAHODHA wa Yanga SC, Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ amesema kwamba wanajutia makosa ya juzi kuwaruhusu Mwadui FC kusawazisha bao dakika za mwishoni na wanawaomba radhi mashabiki wa timu yao.
        Yanga SC ilikaribia kabisa kuvuna pointi tatu juzi Uwanja wa Kambarage Shinyanga baada ya kuongoza kwa 2-1 hadi dakika 87 Mwadui FC iliposawazisha.
        Na matokeo hayo, yanawashushia nafasi ya pili mabingwa hao watetezi katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wakizidiwa kwa pointi mbili na Azam FC ambayo jana iliichapa 4-2 JKT Ruvu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
        “Kwa kweli tunawaomba radhi sana mashabiki wetu kwa makosa ambayo tulifanya juzi, lakini huo ndiyo mpira, ila tutajitahidi tusirudie makosa kama haya,”amesema.
        Cannavaro amesema kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora watawafurahisha mashabiki wao.
        Amesema wanaamini mchezo wa kesho utakuwa mgumu kwa sababu Kagera Sugar ni timu ngumu na japokuwa haina matokeo mazuri, lakini si timu ya kubeza.
        Pamoja na ukweli huo, Cannavaro amesema kwamba watajitahidi wavune pointi tatu katika mchezo huo ili kuweka hai matumaini ya kutetea ubingwa na kurejesha imani ya mashabiki.
        Akiwazungumzia Azam FC, Cannavaro amesema kwamba wanaongoza kwa pointi mbili na ligi bado ndefu na ngumu, hivyo anaamini na wao watateleza mbele ya safari Yanga itapita.
        Yanga SC iliwasili jana usiku Tabora na leo inatarajiwa kufanya mazoezi Uwanja wa Mwinyi kuelekea mchezo wa kesho.
        Kwa ujumla Ligi Kuu inaendelea mwishoni mwa wiki, Jumamosi Simba SC ikimenyana na Majimaji FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga SC na Kagera Sugar Uwanja wa Mwinyi, Tabora, Mtibwa Sugar na Mwadui FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, Prisons na Ndanda FC Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Coastal Union na Mbeya City Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
        Mechi nyingine zitachezwa Jumapili, Azam FC na Toto Africans Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam wakati Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, African Sports itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu wakati Jumatatu, Mgambo Shooting itaikaribisha Stand United.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: YANGA SC WAWAOMBA RADHI MASHABIKI, WASEMA HAWATARUDIA MAKOSA TENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry