// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC INAMBANA MKWASA KUTIMIZA IPASAVYO MAJUKUMU YAKE STARS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC INAMBANA MKWASA KUTIMIZA IPASAVYO MAJUKUMU YAKE STARS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, October 02, 2015

    YANGA SC INAMBANA MKWASA KUTIMIZA IPASAVYO MAJUKUMU YAKE STARS

    Barua ya wazi kwa rais wa TFF.ndugu Jamal Malinzi...
    "Mh rais kwanza nikupongeze sana kwa kazi nzuri ya kuliongoza shirikisho letu la mpira wa miguu nchini.najua ugumu na changamoto unazozipata ktk kazi yako hyo.ila kwa kweli unajitahidi sana hasa kwenye eneo la kuongeza wadhamin kama tulivyoona jana mlipoamua kuingia ktk afya za wachezaji wa ligi kuu kwa kuwapatia bima ya afya.
    Kwa kweli unajitahidi sana rais.
    Kimsingi hii ni barua yangu kwanza kwako rasmi kama mdau wa soka na nitangulize kukuomba radhi kaka yangu kama mawazo yangu yatakuwa hayaendani na unachokiamini ila kama kiongozi wa taasisi nnayoiamini huna budi kuisoma.kwani wakati mwingine hata SAA ILIYOPOTEZA MAJIRA HUONYESHA MUDA SAHIHI.
    Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa anashindwa kuwajibika ipasavyo kwa sababu ya majukumu yake, Yanga SC
     

    ..barua yangu inajikita kwenye muingiliano wa majukumu na mgongano wa kimaslah"conflict of interest"unaomkabili kocha wa sasa wa timu ya taifa ambaye pia ni kocha msaidizi wa klabu ya Yanga Charles Boniface mkwasa.
    Nimeandika muingiliano wa majukumu kwa sababu kuu mbili.
    Ktk hali ya kawaida ni kutoitendea haki klabu ya Yanga na pia kuwanyima Zaid ya haki watanzania kwa kocha mkwasa kutumikia taasis mbili kwa wakati mmoja!
    Yanga ndiyo yenye mkataba na 'master"vp mtu mwenye mkataba naye kila uchwao yupo na timu ya taifa?haki ipi hapa yanga wanaipata?
    Lakini mh rais huyo kocha anaweza kujigawa vp wakati ligi kuu inaendelea?je akae kwenye benchi la ufundi la Yanga au akaangalie wachezaji wa timu nyingine?
    Nimetafiti vya kutosha kwenye hili.kocha Boniface hajawahi kuhudhuria mechi yoyote ya Simba baada ya kuteuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa zaid ya mechi baina ya Simba na yanga ambayo yy ni kocha msaidizi.simaanishi kuwa hapendi kuangalia simba ila muingiliano wa majukumu unambana.
    Na kwa hili nna hakika mechi nyingi za ligi kuu za timu nyingine kocha mkwasa ameshindwa kuhuduhuria na kuona wachezaji wengine zaid ya mechi zinazohusisha timu yake.!!
    Si haki kwa wapenzi wa mpira nchini mh rais!pia ni kuwanyima fursa wachezaji wa klabu nyingine kuangaliwa na kocha wao wa timu ya taifa!
    Lakini pia kuna mgongano mkubwa sana wa kimslahi ambao unamuondolea uhalali'legitimacy"wa kocha mkwasa kutumikia waajiri wawili kwa wakati mmoja...
    Akiwa kocha wa yanga ktk hali ya kawaida ni dhahir shahir chochote atakachofanya hata kama ni kwa nia njema itaonekana anawapendelea wachezaji wa mwajiri wake mkuu yanga!!
    Mfano hai unajionyesha kwa kitendo chake cha kumchagua mchezaji juma Abdul ambaye hapangwi hata kwenye klabu yake ya yanga(juzi kapangwa sababu mbuyu twite ana kadi nyekund)na kuwaacha wachezaji wengine wazuri zaid.au kuwaita ghafla deus kaseke na malimi busungu mara tu baada ya kujiunga na timu ya yanga.ingawa nao bado hawana uhakika wa kuanza kwenye kikosi cha yanga!
    Rais wangu wa mpira kwako ni kufanya maamuzi yenye tija kwa maslahi ya mpira wa miguu nchini.Mkwasa lazma abaki na ajira moja hv sasa. 
    Mwanzo tulielewa ni kazi ya muda tu kule taifa stars ila wenye kuangalia mambo kwa kina hatuoani dalili yoyote ya kuletwa kwa kocha mpya!
    Na pia si vbaya kama amewaridhisha(kama alivyoniridhisha mm)kumpa mkataba wa moja kwa moja na wa kudumu kocha mkwasa ili abaki na ajira moja tu ya Taifa stars kuepusha muingiliano wa majukumu na mgongano wa kimaslahi
    Mh rais mwisho nikutakie kazi njema na nikuombee uzima wa afya na fanaka ili utusogeze mbele kwenye mchezo huu murua zaid duniani,"
    (Imeandikwa na Haji Sunday Manara, Ofisa Habari wa Simba SC)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC INAMBANA MKWASA KUTIMIZA IPASAVYO MAJUKUMU YAKE STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top