// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YAMOTO BAND KUTUMBUIZA SHEREHE ZA RAIS JK NA WANAMICHEZO JUMATATU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YAMOTO BAND KUTUMBUIZA SHEREHE ZA RAIS JK NA WANAMICHEZO JUMATATU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, October 11, 2015

    YAMOTO BAND KUTUMBUIZA SHEREHE ZA RAIS JK NA WANAMICHEZO JUMATATU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BENDI ya Yamoto na Kalunde zinatarajiwa kutumbuiza wakati wa sherehe za Tuzo za Wanamichezo Bora na Tuzo ya Heshima ya Rais Jakaya Kikwete kesho Jumatatu Oktoba 12, 2015.
    Maandalizi kuhusiana na tuzo hizo zinazoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA) yamekamilika kwa kiasi kikubwa na baadhi ya wanamichezo wanaotoka nje ya Dar es Salaam ambao ni miongoni mwa watakaopewa tuzo wanatarajiwa kuwasili leo jioni tayari kwa shughuli hiyo.
    Tunaamini uwepo wa Yamoto na Kalunde itakuwa burudani nzuri kwa watakaohudhuria sherehe hizo, ambapo wachezaji 10 waliong’ara zaidi katika miaka 10 ya Rais Kikwete wanatarajiwa kupewa tuzo.

    Pia TASWA itatoa Tuzo ya Heshima kwa Rais Kikwete pamoja na viongozi watano wa michezo 10 waliofanya vizuri zaidi katika miaka hiyo 10 na pia kutakuwa na tuzo kwa kampuni au taasisi zilizofanya vizuri michezoni kwa muda huo.
    Tukio hilo ambalo pia litahudhuriwa na Rais Kikwete lina lengo pia  la kuwakutanisha wanamichezo na kumuaga Rais Kikwete anayemaliza muda wake kikatiba baada ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 25, mwaka huu.
    Tunawaomba kutokana na ugeni mzito utakaokuwepo katika shughuli hiyo, ni vyema wageni waalikwa wakajitahidi kujali muda kwa kufika kwa wakati ili kuepuka usumbufu mwingine watakaoweza kuupata utakaosababishwa na kuchelewa kuingia kwao ukumbini.
    Wadhamini wa shughuli hiyo itakayoanza saa 12 jioni kwa wageni waalikwa kuanza kuwasili ukumbini ni GSM Foundation,  Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,  Kampuni ya Salim Said Bakhressa (SSB) na Megatrade Investiment.
    Tunawaomba kutokana na ugeni mzito utakaokuwepo katika shughuli hiyo, ni vyema wageni waalikwa wakajitahidi kujali muda kwa kufika kwa wakati ili kuepuka usumbufu mwingine watakaoweza kuupata utakaosababishwa na kuchelewa kuingia kwao ukumbini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YAMOTO BAND KUTUMBUIZA SHEREHE ZA RAIS JK NA WANAMICHEZO JUMATATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top