UHOLANZI imejiweka pagumu kufuzu Euro 2016 nchini Ufaransa, baada ya kufungwa mabao 3-2 na Jamuhuri ya Czech usiku wa jana nyumbani.
Beki wa kulia, Pavel Kaderabek alianza kuwafungia wageni dakika 24 kabla ya Josef Sural kuifungia Czech bao la pili dakika ya 35 kabla ya timu yao kumpoteza Marek Suchy aliyetolewa kwa kadi nyekundu.
Robin van Persie akatokea benchi na kwenda kujifunga dakika ya 66 kuipatia Czech bao la tatu, kabla ya Klaas-Jan Huntelaar kuifungia bao la kwanza Uholanzi dakika ya 70.
Van Persie akafunga bao la pili kwa Uholanzi dakika ya 83, lakini haikusaidia kutokana na Uturuki kuifunga Iceland 1-0.
Uholanzi sasa inaweza kufuzu Euro 2016 iwapo watashinda dhidi ya Czech mchezo ujao na Uturuki watafungwa.
Hii itakuwa mara ya kwanza kikosi cha Danny Blind kushindwa kufuzu fainali za michauno mikubwa tangu mwaka 2002.
Kikosi cha Uholanzi kilikuwa; Zoet, Tete, Bruma, Van Dijk/Dost dk64, Riedewald/Van Persie dk39, Wijnaldum, Blind, Sneijder, El Ghazi/Lens dk69, Huntelaar na Depay.
Mshambuliaji Robin van Persie akisikitika baada ya kujifunga jana Uhoalzni ikichapwa 3-2 na Jamhuri ya Czech PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment