MEI 18, mwaka jana Tanzania ilipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Zimbabwe katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Fainali za Mataifa ya Afrika zilizofanyika mwaka huu nchini Equatorial Guinea.
Mshambuliaji wa Azam FC, John Raphael Bocco aliifungia bao pekee Taifa Stars katika mchezo ambao washambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu walianza.
Mchezo wa marudiano Tanzania ikaenda kulazimisha sare ya 2-2 Harare Juni 1, mwaka jana na siku hiyo mabao ya Stars yalifungwa na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Yanga SC na Ulimwengu.
Tanzania ikasonga hatua ya mwisho ya mchujo ambako ilikutana na Msumbiji, mchezo wa kwanza Dar es Salaam, ililazimishwa sare ya 2-2 Julai 20 na siku hiyo mabao ya Stars wakati huo chini ya kocha Mholanzi, Mart Nooij yalifungwa na kiungo wa Azam FC, Khamis Mcha ‘Vialli’ aliyetokea benchi.
Samatta na Ulimwengu wote walikuwepo uwanjani siku hiyo, lakini walibanwa na labda pengine hawakuwa na bahati na wakashindwa kufunga, ila mwenzao mwingine alifunga.
Mchezo wa marudiano Tanzania ikaenda kufungwa 2-1 Agosti 3 mwaka jana Uwanja wa Zimpeto mjini Maputo, bao la Stars likifungwa na Samatta, lakini matokeo ya jumla yakaitupa nje timu yetu.
Machi 29, mwaka huu Tanzania ililazimishwa sare ya 1-1 na Malawi Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza katika mechi ya kirafiki.
Mchezo huo ambao Stars ilibanwa kipindi chote cha kwanza kabla ya Mrisho Khalfan Ngassa wa Free State Stars ya Afrika Kusini kutokea benchi na kwenda kumsetia Samatta kufunga bao la kusawazisha dakika za lala salama.
Baada ya timu kupitia katika kipindi kigumu chini ya kocha Nooij, hatimaye Jumatano ilipata tena ushindi wa 2-0 dhidi ya Malawi katika mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Siku hiyo, mabao yote ya Stars yalifungwa na washambuliaji wa Mazembe, Samatta na Ulimwengu.
Wakati timu hiyo zinarudiana leo mjini Blantyre, nyumbani kuna maneno yanaendelea kwamba bila Samatta na Ulimwengu, Taifa Stars ‘hakuna kitu’ na Tanzania hakuna wachezaji.
Ni mijadala ambayo imeanzia kwenye mitandao ya kijamii na kupenya hadi kwenye vyombo vya habari.
Wakati mwingine huwa najiuliza, Watanzania huwa tunakosa mada za msingi za kujadili wakati mwingine au vipi?
Maana kila siku ni vihoja tu. Baada ya sare ya 0-0 na Nigeria mechi za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika Septemba 5, wengine wakaanza kusema Taifa Stars inabebwa na Yanga.Tunahitaji elimu ya uzalendo. Elimu ya utaifa.
Tulikemea hilo na wahusika waliomba radhi, lakini tena linaibuka la eti Tanzania bila Samatta na Ulimwengu ‘hakuna kitu’.
Hii inakera kwa sababau moja kubwa, mawazo haya yakiingia ndani ya kambi ya timu ni mabaya na ya hatari.
Wachezaji wengine ambao wanaamini wanajitolea uwanjani kuisaidia timu, watajisikia vibaya.
Lakini hata hao akina Samatta na Ulimwengu, ambao nao wanajua huwa wanacheza na wenzao wengine tisa kwa ushirikiano mkubwa uwanjani, watajisikiaje?
Fikiri kabla ya kutenda, au kusema. Itakusaidia kuepeuka kusababisha hatari kama hizi.
Makala hii inaeleza na kuainisha kwamba Taifa Stars inajivunia wachezaji wake wote wakiwemo Samatta na Ulimwengu, na ndiyo maana kuna mechi wawili hao hawakufunga, wengine wamefunga.
Na itaendelea kuwa hivyo, kuna mechi watafunga, kuna mechi hawatafunga, watafunga wengine.
Sisi Waandishi wa Habari tunatakiwa kuwa mstari wa mbele kuiunganisha timu na wachezaji wetu, wajihisi kitu kimoja na wako sawa, kuliko kuanza kuwatukuza wengine kupita kiasi.
Lakini tunapoanza kuja habari na makala au matangazo ya kuonyesha wachezaji wengine si kitu katika timu ila Samatta na Ulimwengu ni hatari. Tena ni hatari sana.
Tuendelee kuunganisha nguvu zetu kuitakia kia la heri timu yetu ikiingia katika mchezo mgumu leo dhidi ya wenyeji Malawi, ilinde matokeo ya awali Dar es salaam na kusonga mbele. Mungu ibariki Taifa Stars, ibariki Tanzania. Amin.

0 comments:
Post a Comment